Home Habari za michezo FT: YANGA 0-0 CLUB AFRICAIN ….HAKUNA CHA TUISILA WALA AZIZI KI….NABI PRESHA...

FT: YANGA 0-0 CLUB AFRICAIN ….HAKUNA CHA TUISILA WALA AZIZI KI….NABI PRESHA INAPANDA….

DAKIKA 90 za mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Club Africain zimemalizika kwa suluhu (0-0) kwenye uwanja wa Mkapa na hizi ni dondoo zake.

Mwamuzi Celso Armindo Alvacao raia wa Msumbiji hii ilikuwa mara yake ya pili kuchezesha mchezo wa Kimataifa kwenye uwanja wa Mkapa, mara yake ya kwanza ilikuwa Oktoba 7, 2021 wakati Taifa Stars ikiwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Benin.

Ni kadi tatu tu za njano zilitolewa kwenye mchezo huo wa kimataifa zote wakionyeshwa wachezaji wa Club Africain.

Licha ya Yanga kupata kona nyingi zaidi (9) ilishindwa kuzitumia dhidi ya wapinzani wao, Africain (3).

Mchezo wa kwanza kwa Yanga ikiwa nyumbani kwenye uwanja wa Mkapa kutoka suluhu msimu huu kwenye michuano ya kimataifa.
Tangu ajiunge na Yanga ambayo msimu uliopita aliipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la TFF, hii ilikuwa mara ya kwanza kwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi kuiongoza timu hiyo ya Wananchi kucheza dhidi ya timu kutoka kwao Tunisia, Club Africain.

Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga ilipiga mashuti sita huku moja kati ya hayo likilenga lango, Club Africain iliyipiga moja na kulenga lango.

Mpira ulisimama mara 17 kutokana na faulo ambazo zilichezwa na timu zote mbili ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza. Yanga (7), Club Africain (10).

SOMA NA HII  KLABU HII LIGI KUU YAANGAMIA...HALI NI TETE MAAJABU PEKEE NDIO YATAIKOMBOA...ISHU NZIMA IPO HIVI