Home Habari za michezo ISHU YA DROGBA KUBADILI DINI…UKWELI HUU HAPA…SHEKHE ALIYEMSILIMISHA AFUNGUKA A-Z…

ISHU YA DROGBA KUBADILI DINI…UKWELI HUU HAPA…SHEKHE ALIYEMSILIMISHA AFUNGUKA A-Z…

Katika muda wa saa kadhaa, kumekuwa na jumbe nyingi katika mitandao ya kijamii zilizosema kuwa mchezaji maarufu wa zamani kutokaIvory Coast, Didier Drogba, amebadili sini na kuwa Muislamu.

Taarifa hizi zilisambaa baada ya kiongozi mmoja wa Kiislamu anayefahamika kwa jina Dr. Mohamed Salah anayeishi Marekani kuchapisha picha inayoonyeshaDrogba akisali kama Waislamu.

Kasisi huyo alisema kwamba Drogba ameslim, na hivyo ndivyo taarifa hiyo ilivyoenea.

Saa chache baadaye, Bw Drogba alituma ujumbe kwenye mtandao wake rasmi akikanusha madai kwamba alibadilisha dini, na kuongeza kuwa alishangazwa na jinsi taarifa hiyo ilivyosambaa.

“Nilikuwa ninatoa heshima kwa kaka zangu Waislamu na niliokuwa nimewatembelea. Lilikuwa ni tukio ambapo tulionyesha umoja,” alisema Drogba katika ujumbe wake wa Twitter.

SOMA NA HII  'UCHAWI' WA KIBWANA SHOMARI WAMFANYA LOMALISA KUNYOOSHA MIKONO YANGA...