Home Habari za michezo KISA KUISEMEA YANGA…MANARA ‘APIGWA DONGO KIAINA’ NA KARIA…

KISA KUISEMEA YANGA…MANARA ‘APIGWA DONGO KIAINA’ NA KARIA…

Habari za Michezo

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amezionya klabu kwa kutoheshimu adhabu zinazotolewa kwa watumishi wake.

Ametoa onyo hilo jana kwenye mkutano mkuu wa 17 wa kawaida wa Shirikisho hilo ambao umefanyika Jijini Mwanza.

Amesema baadhi ya klabu zinapopewa adhabu hushindwa kuzitekeleza na badala yake kukimbilia kwenye vyombo vya habari huku zikilalamika kuwa adhabu ni kubwa wakati zilishiriki kuzipitisha.

Msemaji wa Yanga, Haji Manara ni mmoja wa waliokumbana na adhabu kutoka TFF hivi karibuni na akaibukia kwenye vyombo vya habari kulalamika huku klabu yake na Rais, Hersi Said wakifunguliwa mashtaka kwa kutoheshimu adhabu hiyo.

“Vilabu tuheshimu maamuzi tuheshimu adhabu zinazotolewa, tunatoa adhabu watu hawaziheshimu. Uzuri ni kwamba adhabu hizi hazifi kuna wakati itafika itakubana tu,”

“Kumekuwa na tabia watu hawatekelezi maamuzi wanakimbilia kwenye media (vyombo vya habari), tutaendelea kusimama kwenye haki na kanuni kwa sababu adhabu hizi zimepitishwa na vilabu vimeshiriki,”

“Mtu yoyote anayetaka adhabu ipunguzwe ina maana anataka afanye makosa, watu wanaoingia kwenye mpira wasome kanuni na sheria, tumepata mafanikio haya kwa sababu tunasimamia kwenye misingi na sheria,” amesisitiza Rais Karia

SOMA NA HII  KLABU HII LIGI KUU YAANGAMIA...HALI NI TETE MAAJABU PEKEE NDIO YATAIKOMBOA...ISHU NZIMA IPO HIVI