Home Habari za michezo PAMOJA NA KUITA WAGANGA WA KIENYEJI…MIKOSI YAZIDI KUMUANDAMA POGBA….

PAMOJA NA KUITA WAGANGA WA KIENYEJI…MIKOSI YAZIDI KUMUANDAMA POGBA….

Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba ni wazi atakosekana nchini Qatar kwenye michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kuanza mwezi huu baada ya kupata majeraha mapya siku kadhaa zilizopita.

Hii imekuja siku chache baada ya kiungo huyo kupona majeraha yake ya goti aliyoyapata mwezi wa nane wakati anajiunga klabuni hapo akitokea klabu ya Manchester United. Lakini taarifa mpya inaeleza kiungo huyo ataendelea kukaa nje ya uwanja baada ya kujitonesha jeraha lake la goti.

Paul Pogba amekua akisumbuliwa na tatizo la goti toka akiwa klabu ya Manchester United jambo ambalo limemfanya amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu. Vilevile kiungo huyo alijiunga na Juventus mwezi wa nane akiwa na majeraha ilielezwa atarudi mwezi wa kumi na ndivyo ilivyokua.

Kiungo huyo ambaye amerudi siku za hivi karibuni baada ya kuuguza majeraha yake na kuwapa matumaini mashabiki wa timu ya taifa ya Ufaransa kua mchezaji huyo amerejea na huenda akawepo nchini Qatar, Lakini habari ya kushtua imetoka na kueleza kiungo huyo ameumia na hataweza kuwepo nchini Qatar kuiwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya kombe la dunia.

Kiungo Pogba ataungana na kiungo mwenzake wa kimataifa wa Ufaransa Ngolo Kante ambae nae atakosekana kwenye michuano hiyo mwaka huu. Huku wakiacha pengo kwani hawa ni miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi kwenye timu hiyo wakati Ufaransa wanakua mabingwa mwaka 2018.

SOMA NA HII  ISHU YA MAXI KUTAKIWA SIMBA UKWELI HUU HAPA...TIMU YAKE YA CONGO WAANIKA KILA KITU...