Home Habari za michezo PRESHA YA MABEKI YASHUKA YANGA…BANGALA AMTULIZA NABI…MBEYA CITY KAZI WAPAGAWA HUKO..

PRESHA YA MABEKI YASHUKA YANGA…BANGALA AMTULIZA NABI…MBEYA CITY KAZI WAPAGAWA HUKO..

Kiraka wa Yanga, Yannick Bangala anarejea kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City baada ya kumaliza adhabu ya kukosa mchezo mmoja kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Bangala anarejea wakati ambao Nabi anamhitaji zaidi kutokana na nahodha wake, Bakari Mwamnyeto kupata majeraha kwenye mchezo uliopita wa Ligi dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Liti mjini hapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yote yakifungwa na Fiston Mayele.

Nabi ilimbidi kufanya mabadiliko kwa kutoa Mwamnyeto ambaye alishindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ilichukuliwa na Ibrahim Bacca ambaye alicheza sambamba na Dickson Job.

Urejeo wa Bangala utaongeza nguvu kwa Yanga katika beki yao ya kati kufuatia kuumia kwa Mwamnyeto ambaye uchunguzi zaidi wa kitabibu utabainisha atakuwa nje ya uwanja kwa muda.

Akizungumzia urejeo wa Bangala, Nabi alisema ni mchezaji muhimu na anatarajia kuwa kwenye mipango yake kwa ajili ya michezo ijayo ambayo ni dhidi ya Mbeya City na Ihefu, mchezo na Mbeya City utachezwa Novemba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

“Nimekuwa nikitoa nafasi kwa kila mchezaji kutoa mchango wake, ni muhimu muda mwingine kufanya mabadiliko ya wachezaji ili kupata muda wa kupumzika,” alisema.

Nabi amekuwa akifanya mabadiliko karibu kwenye kila nafasi ya kikosi chake cha kwanza yakiwemo ya lazima mfano kipa wake namba moja Djigui Diarra ambaye alikuwa na majukumu ya timu yake ya taifa la Mali hivyo Abutwalib Mshery ameingia kikosini na kufanya vizuri.

Eneo la beki ya kati na kuna muda huanza Dickon Job na Bangala au Mwamnyeto hata upande wa beki ya kulia na kushoto ambako kwa sasa anafanya vizuri Joyce Lomalisa.

SOMA NA HII  KISA SIMBA...NABI ABADILI SILAHA ZA MAANGAMIZI YANGA...SIMBA YAWAINGIZA CHAKA WAARABU..MORRISON AFICHWA..