Home Habari za michezo KISA YANGA….MANULA ‘AWACHANA LIVE’ MASTAA WENZAKE SIMBA…

KISA YANGA….MANULA ‘AWACHANA LIVE’ MASTAA WENZAKE SIMBA…

Habari za Simba leo

Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema ili kulirudisha taji la Ligi Kuu msimu huu ni lazima wachezaji wajitoe kwa ajili ya timu.

Kipa huyo amesema wachezaji wenzake wa Simba ni lazima wacheze kwa bidii kutokana na ushindani uliopo kutoka Yanga na Azam.

Manula amemaliza mzunguko wa kwanza akiongoza kwa kutoruhusu bao mara sita katika michezo 11 aliyodaka kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi.

“Ligi ya msimu huu imezidi kuwa ngumu ndio maana nikasema mbali ya mbinu kutoka kwa benchi la ufundi lakini ni vyema kila mchezaji akatimiza wajibu wake ndani ya uwanja,” alisema Manula.

Kipa huyo amesema wajibu huo usiangalie kwenye ligi kuu peke yake bali hata mashindano ya kimataifa.

SOMA NA HII  TANO BORA YA UTUPIAJI, SIMBA WATAWALA