Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKIWAZA PA KUMPELEKA…MBEYA CITY WAMKATAA KIBU DENIS MAZIMA…

WAKATI SIMBA WAKIWAZA PA KUMPELEKA…MBEYA CITY WAMKATAA KIBU DENIS MAZIMA…

Habari za Simba

Benchi la ufundi la Mbeya City limeweka wazi kuwa hawana mpango wa kumrudisha kwenye timu yao, Kibu Denis.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya klabu ya Simba kabla ya kujiunga nao alikuwa akikitumikia kikosi cha Mbeya City kwa mafanikio makubwa.

Akizungumzia hilo, Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema โ€œKwanza benchi la ufundi halijatoa mapendekezo yeyote juu ya usajili.

โ€œLabda hilo lipo kwa Uongozi lakini kwa sasa kocha amesafiri kwenda kuisalimia familia yake hivyo tunamsubiri akifika yeye ndio atatoa mapendekezo yake.โ€

SOMA NA HII  MASOUD DJUMA AANZA KWA MKWARA MZITO DODOMA JIJI...AWAKIMBIZA WACHEZAJI MCHAKAMCHAKA JUANI...