Hatimaye kwa mara ya kwanza kiungo mshambualiaji wa Simba SC Saido Ntibazonkiza leo amejumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya jioni ikiwa ni siku moja toka atangazwe.
Saido ambaye niusajili mpya na wa kwanza kwa Simba SC toka kufunguliwa kwa dirisha doho la usajili tarehe 15 mwezi huu, amejiunga na timu hiyo ambayo iko Mwanza ikijiandaa kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC hapo kesho.
Zifuatazo ni sehemu ya picha za tukio hilo, ambapo zinamuonyesha Saido akiwa na furaha kujiunga na Simba SC akiwa ni sehemu ya wachezaji wachache wa kigeni ambao wamepata nafasi ya kucheza Simba na Yanga .


Kulingana na mazoezi ya leo, huenda kesho Kaimu Kocha MKuu wa Simba , Juma Mgunda akashawishika kumuanzisha katika kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya KMC.
