Home Azam FC KAMA UTANI VILEE…AZAM FC WAHAMIA SIMBA SC…KAKOLANYA ‘AUNDIWA KAMATI’….

KAMA UTANI VILEE…AZAM FC WAHAMIA SIMBA SC…KAKOLANYA ‘AUNDIWA KAMATI’….

Golikipa wa Simba SC chaguo la Pili David Kakolanya kujiunga na Azam FC

Imefajamika kuwa, Azam FC, imeanza mazungumzo ya kimyakimya kwa ajili ya kuipata saini ya kipa namba mbili wa Simba SC, Beno Kakolanya.

Kakolanya hivi sasa amekuwa hana nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Simba SC, huku mkataba wake ukitajwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Taarifa zinasema kwamba, yapo mazungumzo ya siri yanayofanywa kati ya kipa huyo chaguo la pili ndani ya kikosi cha Simba SC  na mabosi wa Azam FC.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uzoefu na ubora alionao Kakolanya, ndio umewashawishi Azam FC kumfuata kwa ajili ya kumsajili.

Aliongeza kuwa, kama mazungumzo hayo yakifikia hatua nzuri, basi Kakolanya atasaini mkataba wa kuichezea Azam .

“Tumepanga kukifanyia maboresho kikosi chetu katika usajili huu wa dirisha dogo.

“Tayari tupo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji, kati ya hao yupo Kakolanya ambaye tumeanza naye mazungumzo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe, alizungumzia usajili kwa kusema kuwa: ” Tumepanga kufanya usajili mkubwa katika dirisha dogo wa kimyakimya, watu hawataamini.”

Azam  inatajwa kuwa kwenye wakati wa kusaka kipa mwingine baada ya kipa namba moja wa kikosi hicho, Ali Ahmada raia wa Comoros kuonekana kutofiti eneo hilo.

SOMA NA HII  CLATOUS CHAMA AWEKA REKODI YAKE KIMATAIFA