Home Habari za michezo SAKATA LA FEI TOTO KUVUNJA MKATABA….JEMEDARI SAID AILIPUA TENA YANGA SC…

SAKATA LA FEI TOTO KUVUNJA MKATABA….JEMEDARI SAID AILIPUA TENA YANGA SC…

Jemedari saidi awananga Yanga SC

Mchambuzi wa Soka la Bongo na Kimataifa Jemedari Said Kazumari ameibuka na kupinga maamuzi yaliyotangazwa na baadhi ya Wazee wa Klabu ya Yanga SC jana Jumatano (Desemba 28).

Wazee wa Yanga SC waliitisha Mkutano na Waandishi wa Habari na kueleza namna walivyosikitishwa na kitendo cha Kiungo Feisal Salum kutishia kuondoka Klabuni hapo, huku Azam FC ikitajwa kuhusika kwenye sakata hilo.

Wazee hao walikwenda mbali zaidi na kutangaza maazimio na kuwa tayari kutonunua tena bidhaa za Makampuni ya SSB (Said Salim Bakhresa) kwa kuonesha wamechukizwa na wanachodhaniwa kukifanya kwa Fei Toto, japo Uongozi wa Azam FC umekanusha kuhusiska na mpango huo.

Huku wakianika wazi kuwa hata kama wanakusudia kufanya hivyo, zipo taratibu za wao kufuata na si kama inavyosemwa kwemye mitandao.

Jemedari ameibuka leo Alhamis (Desemba 29) na kuandika ujumbe mzito katika Mitandao ya Kijamii na kuupa Kicha cha Habari kisemacho β€˜HII NCHI INA WAJINGA WENGI SANA’.

β€œKwani bado HAJAFIKA tu kambini AVIC TOWN? Si tunaambiwa ameomba na msamaha na KUKIRI kosa?

Nchi ya wajinga, ujinga umetamalaki, ujinga umeshika usukano na unaongoza njia, viongozi wa nchi ya wajinga wanatumia ujinga wa wananchi wao kama MTAJI katika kuficha madhaifu yao.

Nyakati hizi za kilo ya mchele 3,000 -3,500 (Afutatu , mpaka Afutatu miatano), maharage kilo 3,400 (Afutatu mianne) na vyakula vingine bei zikiwa zimepanda sana. Kuna ujinga wa kuambiana usinunue CHAKULA kwa yule kisa wamesajili mchezaji wetu.

Watu wenyewe tunakula TUNACHOKIONA sio TUNACHOKITAKA halafu tuongezewe na ujinga wa kuchagua anauza fulani usinunue. Ukiuliza kisa nini wamemchukua mchezaji wetu.

Wakati huo huo Uongozi wa Yanga SC umetuma barua ya kiofisi kuomba kusajili wachezaji 2 wa Azam FC. Huku kwenye nchi ya wajinga ambako ujinga umetamalaki tunaambiwa tusinunue bidhaa zao kisa kuna wajinga wenzetu wanasema Azam wanamtaka FEI.

Katika nchi ya wajinga pekeyake ndiko ambako wananchi tunaaminishwa mpira sio biashara mpaka pale sisi tunapotaka kununua au kuuza. Wenzetu wakitaka kwetu haikubaliki.

WAJINGA NDIO WALIWAO.

SOMA NA HII  SIMBA vs WYDAD NI KISASI NA HESHIMA MASTAA WATOA TAMKO