Home Habari za michezo KASEKE AIBUKA NA HILI JIPYA KUHUSU KAGERE…AANIKA A-Z SIRI ZAKE…

KASEKE AIBUKA NA HILI JIPYA KUHUSU KAGERE…AANIKA A-Z SIRI ZAKE…

Kaseke akiwa Singida Big Stars

Winga machachari wa Singida Big Stars, Deus Kaseke amefichua kucheza na mastaa wengi kikosini akiwamo straika Meddie Kagere imemrahisishia sana kazi na watafanya makubwa msimu huu.

SBS imekuwa na matokeo mazuri ikiwa nafasi nne za juu kwa pointi 30 huku Kagere akiongoza kikosini kwa idadi kubwa mabao (matano) tangu ajiunge na matajiri hao wa mkoani Singida.

Hata hivyo, katika mechi nyingi, Kaseke ameonekana kuwa na maelewano mazuri uwanjani na straika huyo wa Kinyarwanda na kufanya safu ya mbele kuwa imara na bora zaidi.

Akizungumza jijini hapa, Kaseke aliyewahi kutesa Mbeya City na Yanga alisema tangu kutua kikosini humo, anafurahia sana muunganiko wa timu kwa kila mchezaji kucheza kwa malengo.

“Siri kubwa yangu na Kagere ni kuanzia mazoezini siyo kwenye mechi tu, tunachofanya ni kupambania ubingwa na zaidi nafurahia wachezaji wote kila mmoja anajituma na kufanya tuwe na muunganiko imara,” alisema Kaseke.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm alisema anafurahishwa na mwenendo wa timu hiyo akibainisha kuwa baada ya kukamilisha saini ya winga, Nickson Kibabage (Mtibwa Sugar) anasaka wengine wawili.

“Lazima niongeze wengine wawili eneo la beki wa kati na straika nahitaji kuona timu ikicheza soka la kasi na mabao mengi ligi ni ngumu haswa wakati huu wa raundi ya pili,” alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga.

SOMA NA HII  MOLOKO, AUCHO NA NGUSHI WARUDISHA 'UTUKUFU' YANGA...WAANZA UPYA KWA KASI YA 'KIMONDO'...