Home Habari za michezo KAZE : HII YANGA KAMA SIO AUCHO NA FEI TOTO HALI...

KAZE : HII YANGA KAMA SIO AUCHO NA FEI TOTO HALI INGEKUWA SIO…

Yanga imerejea jijini Dar es Salaam kutoka Lindi ilipokwenda kucheza mechi ya kufungia duru la kwanza la Ligi Kuu dhidi ya Namungo, huku kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze akifichua kilichowabeba kushinda kwa mara ya kwanza ugenini dhidi ya Wauaji wa Kusini na kuwataja viungo, Khalid Aucho na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Yanga ilishinda mabao 2-0, yaliyowekwa kimiani na Yannick Bangala na Tuisila Kisinda na kuipa ponti tatu zilizoifanya ifikishe 38 na kujikita kileleni mwa msimamo, huku Kocha Kaze akiisimamia timu hiyo baada ya kocha mkuu, Nasreddine Nabi kusimamishwa mechi tatu kwa utovu wa nidhamu.

Kabla ya ushindi huo, Yanga ilishakutana na Namungo mara sita na kushinda mara moja tu nyumbani wakati mechi nyingine tano za nyumbani na ugenini zikiisha kwa sare na juzi ilikuwa mara ya kwanza kushinda ugenini dhidi ya timu hiyo iliyopanda daraja misimu mitatu iliyopita.

Kocha Kaze amesema kazi kubwa iliyofanywa na viungo hao wawili wakishirikiana na wenzao, ndiyo siri kubwa iliyowabeba dhidi ya Namungo, huku akikiri pambano lilikuwa gumu, lakini liliamuliwa na ubora wa eneo la kiungo lililokuwa na mafundi hao, Aucho na Fei Toto.

Kaze alisema Aucho na Fei walicheza vyema kama pacha na kuivuruga kabisa Namungo, huku wakiwa wepesi kuichezesha timu kwa dakika zote 90.

“Mbali na kazi kubwa ya viungo hao, lakini hata ukiangalia mchezo, mashambulizi mengine tuliyoyafanya yalikuwa yakitumika pembeni kwa mawinga na walifanya vizuri mno kama ilivyokuwa kwa mabeki ambao nawapongeza kwani kuna muda timu ilikuwa chini, lakini wao walikuwa imara kuhakikisha tunakuwa salama,” alisema Kaze aliyeugusia pia Uwanja wa Majaliwa.

Kocha huyo raia wa Burundi, alisema uwanja huo ulikuwa rafiki kwao kucheza mpira wao ambao wanaucheza.

SOMA NA HII  SIMBA KUKUTANA NA VINARA HAWA...LIGI YA MABINGWA AFRIKA