Home Habari za michezo KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA….VIGOGO WASUSIA NAFASI YA UENYEKITI….

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA….VIGOGO WASUSIA NAFASI YA UENYEKITI….

Kamati ya Uchaguzi wa Simba ilifungua mlango kwa wagombea kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali tangu Desemba 5, mwaka huu lakini hadi jana Jumamosi hakuna mgombea aliyejitokeza kuchukua ya uenyekiti.

Nafasi ya mwenyekiti ambayo inawaniwa ipo chini ya Murtaza Magungu ambaye alichaguliwa kwenye uchaguzi mdogo baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi kujiuzuru.

Ni wajumbe wanne pekee wamechukua fomu hizo ambao ni Abubakari Zebo aliyechukua Desemba 6, Abdallah Rashi Mgomba, Hawa Mwaifunga na Iddy Noor Kajuna waliochukua Desemba 7.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Boniface Lihamwike alisema kuwa bado kuna muda kwa wenye nia ya kuwania nafasi hizo kwani mwisho ni Desemba 19.

Simba wanafanya uchaguzi huo baada ya viongozi waliopo madaraka kuongoza kwa miaka minne kwa mujibu wa katiba. Nafasi zinazowaniwa ni mwenyekiti na wajumbe wanne pekee.

Kwa mujibu wa katiba yao, mwenyekiti atakayechaguliwa ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili ambao wataingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi wakitimiza idadi ya wajumbe saba kutoka upande wa klabu kuingia katika bodi hiyo.

“Hakuna aliyechukua fomu upande wa mwenyekiti hadi sasa. Majina niliyonayo ni hayo manne ambao ni Kajuna, Mgomba, Hawa na Zebo, naamini wataendelee kujitokeza kwani muda upo,” alisema Lihamwike ambaye ni Hakimu Mkazi wa Kiteto mkoani Manyara.

SOMA NA HII  'JUJU' ZA MBOMBO ZAMPAGAWISHA ONGALA AZAM FC...HASIKII WALA HAAMBILIKI KWAKE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here