Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

MIQUISSONE AIWEKEA NGUMU SIMBA….AGOMA KUPUNGUZA MSHAHARA WAKE…

admin July 4, 2023 8:32 pm

Simba huenda ikaachana na mpango wa kumsajili winga Luis Miquissone baada ya kushindwa kufikia nae makubaliano ya mshahara.

Kulingana na mwanahabari maarufu wa Ghana Micky Junior, Miquissone ameweka ngumu kupunguza mshahara wake

Al Ahly wako tayari kumuuza au kumtoa kwa mkopo katika timu ambayo itagharamia mashahara wake kwa asilimia 100%

Lakini imeonekana mshahara wake (karibu Mil 95 kwa mwezi) ni tatizo sio kwa Simba tu, klabu nyingi zilizoonyesha nia ya kumuhitaji awali, zimejiondoa

Inaaminika kuwa Miquissone hataki kutolewa kwa mkopo na Al Ahly huku kukiwa hakuna ofa iliyowasilishwa kutaka kumnunua

Winga huyo wa Kimataifa wa Msumbiji, anataka Al Ahly wavunje mkataba wake kama hawataki kuendelea nae ili awe mchezaji huru

Kama Al Ahly watavunja mkataba wao ina maana watamlipa gharama zote na atakuwa huru kufanya mazungumzo mapya na klabu nyingine

‘BEKI LA CHAN’ NA YANGA NI SUALA LA MUDA TU….MWENYEWE AANIKA A-Z ISHU ILIVYOPIGWA.. WAKATI UKINGOJA LIGI ZIRUDI…ENDELEA KUFURAHIA MTONYO KUPITIA MERIDIANBET…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “MIQUISSONE AIWEKEA NGUMU SIMBA….AGOMA KUPUNGUZA MSHAHARA WAKE…”

  1. Nassoro Juma says:

    Lolote linawezekana

Leave a Reply