Home Habari za michezo SIMBA SC WAPEWA MCHONGO WA UBINGWA BONGO…WATAKAO SAJILIWA HAWA HAPA…

SIMBA SC WAPEWA MCHONGO WA UBINGWA BONGO…WATAKAO SAJILIWA HAWA HAPA…

Habari za Simba

Wachezaji wa zamani wa Simba SC wameitaka klabu hiyo kusajili wachezaji wawili muhimu ambao ni mshambuliaji na kiungo mchezeshaji ili waweze kutoboa kwenye michuano mbalimbali inayowakabili mwakani.

Simba SC juzi ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu na kufikisha pointi 38 huku ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi nyuma ya vinara na mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 44.

Kiwango cha timu hiyo kwa siku za karibuni kimeonekana kama hakiwaridhishi mashabiki wa klabu hiyo licha ya kwamba kuna mechi wanashinda kwa mabao mengi.

Beki na nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Boniface Pawasa alisema Simba SC inahitaji haraka kusajili mshambuliaji na kiungo mchezeshaji ili kuweza kuwasaidia waliopo katika mashindano yanayowakabili kwa sasa.

“Waongeze mtu mmoja wa kuwasaidia Phiri na Bocco kwa sababu ukiangalia huko mbele wana mashindano mengi sasa kwa jinsi wanavyocheza sasa na bila kujipanga wanaweza wasitoboe.

“Tumeona baadhi ya wachezaji wakikosekana timu inayumba unaiona kabisa timu inasumbuka kupata matokeo hivyo wanatakiwa pia kuongeza kiungo mshambuliaji mahiri pale kati ili aweze kuichezesha timu,” alisema Pawasa na kuongeza;

“Pia ikiwezekana hata beki hasa wa kushoto wanatakiwa kuongeza ili kumsaidia Mohammed Hussein ’Tshabalala’ kwani kama mchezaji huyo atapata majeraha makubwa timu lazima ipate mtikisiko.

Naye beki mwingine wa zamani wa klabu hiyo, Qureish Ufunguo, alisema timu hiyo haina budi kutafuta mshambuliaji (namba 9) na kiungo mchezeshaji ili kuleta ufanisi katika kikosi.

“Sio kwamba waliopo ni wabaya, hapana lakini lazima wapatikane wengine mbadala tena wazuri zaidi ya waliopo ili kuongeza ufanisi ndani ya kikosi maana wakati mwingine unaangalia timu inavyocheza unaona kabisa kunahitajika nguvu nyingine ya ziada ili kurejesha ubora wa Simba SC,” alisema Ufunguo.

Simba SC kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ikiwa na pointi 38, zikiwa ni sita nyuma ya vinara Yanga ambayo ina pointi 44 na keshokutwa itacheza na Azam kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na Simba inacheza dhidi ya KMC, CCM Kirumba Mwanza.

SOMA NA HII  HII YANGA IMESHAKUWA BALAA, KOCHA CR BELOUIZDAD AITAJA KENYE HILI