Home Azam FC MASTAA AZAM FC WAFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA YANGA SC…MMOJA ACHOMOA…

MASTAA AZAM FC WAFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA YANGA SC…MMOJA ACHOMOA…

Yanga SC kusajili mastaa Azam FC

Mapema wiki iliyopita Yanga SC ilituma barua Azam FC ya kutaka mazungumzo ya kuwapata wachezaji wake wawili, kiungo Mghana James Akaminko na winga Muivory Coast Kipre Junior jambo ambalo hadi sasa ni gumu kutimia kutokana na sababu mbalimbali.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alithibitisha kupokea barua hiyo na kueleza kuwa wataijibu baada ya mechi ya jana dhidi ya Mbeya City, lakini tayari Akaminko ameweka bayana kwamba hana uhakika kama dili hilo litatiki kwa vile anabanwa na mkataba wa mabosi wake wa sasa.

Wachezaji hao wawili na kila mmoja ameweka wazi kusikia taarifa hizo na kufunguka uamuzi wake.

“Nimesikia taarifa hizo, lakini siwezi kueleza chochote bali uongozi wangu (Azam FC) ndio unajua kila kitu. Kazi yangu ni kucheza soka na naendelea kupambana ili kuhakikisha timu inafikia malengo hayo mengine sio kazi yangu kuyazungumzia,” alisema Akaminko.

Alipoulizwa kama anaweza kujiunga na Yanga SC, alisema hawezi kuzungumzia, ila anahisi kwamba itakuwa ngumu kwake kwa vile ndio kwanza ameingia mkataba hivi karibuni na pia kiu yake ni kuitumikia kwa muda mrefu na kuipa mafanikio kwa kitendo cha kuaminiwa na kufuatwa kwao Ghana.

Kwa upande wa Kipre alisema: “Nimefurahi kuona hizo tetesi pia nimezichukua kwa mtazamo chanya kwani ni heshima kwangu. Pamoja na yote nimeichukua kama chachu ya mimi kufanya vizuri na kuonekana zaidi kwani hata hapa bado sijaonyesha ubora wangu kwa asilimia 100. Ni hayo tu, mengine waulize wahusika.”

Hata hivyo,  kuwa Azam SC imepanga kuwajibu Yanga SC na kuwapa bei ya wachezaji hao ambapo pesa ya kumnunua mmoja tu sio chini ya Dola 400,000 zaidi ya Sh900 milioni za Kibongo na hapo bado dau binafsi la usajili kwa mchezaji na mshahara itakaokuwa inamlipa kila mwezi pamoja na maslahi mengineyo.

Yanga SC ilitangaza kuwataka wachezaji hao siku chache baada ya kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuvunja mkataba na kuilipa klabu hiyo Sh112 milioni kama ilivyo kwenye vipengele vya mkataba huo ili awe huru kujiunga na timu nyingine na Azam ikitajwa ndio inayomnyemelea.

SOMA NA HII  BEKI KISIKI WA SIMBA APIGWA STOP KONGO

1 COMMENT

  1. kwani ninyi mnajua kikao cha azam kitakuja na nini mpaka mpange kiasi cha pesa ambacho AZAM watawambia Yanga ,poleni Timu yenu Simba ni mbovu cse scounting yake utegemea waandishi wa mpira na ninyi hamjui lolote kuhusu wacchezaji ,watateseka sana ndiyo maana sasa wameangukia kwa SAIDO,hapa mnavizia FEI .