Home Habari za michezo KISA USAJILIWA DOUMBIA….BIGIRIMANA ATAKA MKWANJA WAKE WOTE YANGA….ATUMA BARUA NZINTO…..

KISA USAJILIWA DOUMBIA….BIGIRIMANA ATAKA MKWANJA WAKE WOTE YANGA….ATUMA BARUA NZINTO…..

Habari za Yanga

Yanga ilifunga usajili kwa kumtambulisha beki kisiki raia wa Mali, Mamadou Doumbia aliye na timu yake ya taifa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani ‘CHAN’ zinazoendelea nchini Algeria huku usajili wa kitasa hicho ukimng’oa kiungo Gael Bigirimana kwa Wanajangwani hao.

Katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Jumapili Januari 15 imesajili wachezaji wanne, wawili wazawa na wawili wa kigeni lakini ili wageni hao waingie walihitaji kupungua wengine wawili kutoka kwa waliokuwepo awali ili kutimiza idadi inayotakiwa ya mapro 12.

Tayari Yanga ilifanya maamuzi magumu kwa kuachana na mshambuliaji wake, Mkongomani Heritier Makambo na nafasi yake ikazibwa na straika Kennedy Musonda aliyetokea Power Dynamos ya kwao Zambia ambaye yuko moto sasa akiwa na mabao 11 msimu huu akiongoza kwa kucheka na nyavu kwenye ligi ya huko lakini ugumu ukaja kwenye nani mwingine atoke ili kumpisha Doumbia ambaye ni mapendekezo ya benchi la ufundi.

Hapo ndipo uongozi wa Yanga uliumiza kichwa kwani mezani kwao walikuwa na majina matatu ya mawinga wawili Tuisila Kisinda na Jesus Moloko na kiungo Bigirimana lakini hata hivyo kocha mkuu wa kikosi hicho Nassredine Nabi aliwaambia anamipango na Kisinda na Moloko hivyo wahakikishe hawaondoki.

Kwa kauli hiyo ya Nabi, viongozi wa Yanga wakabaki na jina moja tu la Bigirimana mezani lakini wakawa wanahofia kumuacha kwani itawalazimu kumlipa mkwanja mrefu kutokana na mkataba aliosaini lakini mwisho wa siku wakafumba macho na kuamua kumchomoa huku wakiwa tayari kumlipa.

Maamuzi hayo pia yalifanyika usiku wa juzi masaa matatu kabla ya usajili kufungwa ndipo ikamtangaza beki Doumbia saa 6:01 usiku, dakika moja baada ya usajili kufungwa.

Hata hivyo, moja ya watu wa karibu wa Gael, alisema kuwa tayari wametuma barua ya kuhitaji malipo ya kuvunja mkataba na mengine ya nyuma ili mchezaji huyo aondoke zake Dar es Salaam na kutafuta maisha mengine akitarajiwa kurudi nchi kwao Burundi kisha England ambako ndiko makazi na familia yake iliko.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO PACOME ANAVYOTUMBUA MSHAHARA WA YANGA KISHUA....