Home Habari za michezo BEKI RUVU SHOOTING AFUNGUKA ISHU YA KUJIFUNGA DHIDI YA YANGA…AMTAJA ALIYENYUMA YA...

BEKI RUVU SHOOTING AFUNGUKA ISHU YA KUJIFUNGA DHIDI YA YANGA…AMTAJA ALIYENYUMA YA PAZIA…

Habari za Yanga

Tukio la kujifunga kwa beki wa Ruvu Shooting, Mpoki Mwakinyuke dhidi ya Yanga, juzi Jumatatu Uwanja wa Benjamin Mkapa, anatajwa straika mpya wa Yanga, Kennedy Musonda ndiye kasababisha.

Juzi Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo wa Ligi Kuu Bara na kuendelea kuongoza msimamo huku wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Gazeti la Mwanaspoti lilimtafuta Mwakinyuke kujua kitu kilichosababisha presha ya kurejesha mpira kwa kipa wake, Isihaka Hakimu, aliyeshindwa kuudaka na alisema sababu mojawapo ya kujifunga ni kumhofia Musonda.

β€œKuna mambo mawili yaliyosababisha hilo, lengo nilikuwa nataka kuupiga mpira nje.

β€œJambo la pili Musonda alikuwa anakuja kwa kasi na alikuwa karibu kabisa na mpira na ningechelewa kidogo angefunga, hivyo nilitaka nipige nje angalau wapate kona ambayo tungepata muda wa kujipanga kuokoa kuliko angepiga moja kwa moja eneo lile angefunga bao, basi kwa bahati mbaya nikajifunga.”

Alisema anaona namna mashabiki wanavyomwandama kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakikumbusha ile kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Simba akiwa na Mbeya City, lakini haoni sababu ya kujibizana nao zaidi ya kurekebisha makosa yake na kuwa bora zaidi.

β€œKuna wengine wananitumia ujumbe kwamba asante sana kwa kutupa pointi tatu Yanga, inaniumiza sana, laiti kama wangekuwa wao sijui wangefanya nini ile sehemu, kiukweli wachezaji wa nje wana akili ya ziada usipomdhibiti mapema mnaweza kuadhibiwa sana.

Kipa wa timu hiyo, alimkingia kifua Mwakinyuke hata baada ya kumfunga aliongea naye atulie ni makosa ya kawaida kwenye soka na siyo wa kwanza kujifunga.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUCHAPWA NA KAGERA JUZI...PABLO ATIKISA KICHWA KISHA ASEMA HAYA...ADAI KUUMIA...