Home Habari za michezo KISA BANDA KUANZA MATIZI SIMBA…SAKHO ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA MENGI YA NYUMA YA PAZIA..

KISA BANDA KUANZA MATIZI SIMBA…SAKHO ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA MENGI YA NYUMA YA PAZIA..

Habari za Simba

Pape Othman Sakho amesema anafuraha kubwa kumuona Jerry wake, Peter Banda anarejea dimbani tayari kuitumikia klabu yao ya Simba SC.

Sakho ameyasema hayo wakati yeye pamoja na wachezaji wenzao walipokuwa kwenye mazoezi ya kujiandaa dhidi ya mchezo wao wa Kombe la Azam Federation Novemba 28, 2023 dhidi ya Coastal Union.

“Amekuwa muda kwa mrefu, nilimmisi sana. Nilimisi asist zake, nilikuwa nikimtia moyo maana alikuwa anajisikia vibaya kuona sisi tunacheza wakati yeye hawezi kucheza kutokana na majeraha.

“Sasa yupo fiti ameshakata kitambi kama unavyomuona, kwa kweli nafurahi kumuona amerudi,” alisema Sakho.

Banda ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi mitatu tangu apate majeraha Novemba 29, 2022 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Big Stars, anatarajia kurudi rasmi kwenye mechi za ushindani wiki ijayo.

SOMA NA HII  JICHO LA NABI LAANGUKIA KWA MASTAA HAWA 3 WA YANGA....ANAWEZA KUWASAJILI..? JIBU HILI HAPA..