Home Habari za michezo JINA LA SAMATTA LATAJWA AL AHLY YA MISRI…WAARABU WATAKA KUPINDUA MEZA KIBABE…

JINA LA SAMATTA LATAJWA AL AHLY YA MISRI…WAARABU WATAKA KUPINDUA MEZA KIBABE…

Samatta

Al-Ahly ya Misri imeripotiwa kuwa katika mpango wa kumsajili nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta wakati wa majira ya usajili wa mwezi Januari.

Vigogo hao wa Cairo kwa sasa wanatafuta mshambuliaji wa kati na chaguo lao la kwanza ni Mkongomani Jackson Muleka.

Hata hivyo, Muleka anayekipiga na Besiktas anadaiwa kutaka kiasi kikubwa cha fedha kujiunga na miamba hiyo barani Afrika.

Lakini endapo watamkosa, bado jicho lao la pili lipo kwa Samatta anayekipiga na Genk akitokea Fenerbahce kwa mkopo.

Kwa mujibu wa Sporx, Fenerbance wana mpango wa kuachana na Samatta kwa sababu hayupo katika mipango ya kocha Jorge Jesus. Samatta anaripotiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 2.7.

Kuna uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe aliyewahi pia kuichezea Aston Villa akajiunga na timu hiyo kwa sababu Al- Ahly wanahitaji kuwa na mshambuliaji wa kati mapema iwezekanavyo kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia la vilabu linaloanza mwezi ujao.

Samatta amefunga goli moja tu katika mechi 15 alizocheza katika ligi ya Ubelgiji, maarufu Jupiter Pro league.

SOMA NA HII  KUHUSU SIMBA DAY KUPELEKWA MBAGALA ZAKHEM...AHMED ALLY AFUNGUKA SABABU NA MIKAKATI ILIVYO....