Home Uncategorized KUHUSU SHIBOUB KURUDI SIMBA..UKWELI WA MAMBO HUU HAPA..!!

KUHUSU SHIBOUB KURUDI SIMBA..UKWELI WA MAMBO HUU HAPA..!!

MAMBO yameendelea kuwa magumu kwa kiungo wa Simba, Shaaraf Shiboub ambaye yupo kwao Sudan kutokana na janga la corona hivyo, marufuku ya watu kutoka imeendelea kuchukua nafasi hadi Juni 29, mwaka huu.

Awali, ilitarajiwa kuwa huenda mara baada ya marufuku ya mwanzo kufikia ukomo pengine kiungo huyo mkabaji angerejea nchini kwa ajili ya kuungana na wachezaji wenzake kuupigania ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Mambo yamekuwa tofauti baada ya marufuku ya mwanzo kufikia ukomo, viongozi wa taifa hilo wameamua kupanua kizuizi katika jimbo la Khartoum hadi Juni 29, zote hizo ni juhudi za kupambana na janga la virusi vya corona.

Baraza  la Usalama na Ulinzi nchini humo liliweka wazi, Jumatano hivyo Simba ambao walicheza jana mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui, wataendelea kukosa huduma ya Shiboub katika mchezo yao mitatu ijayo.

Michezo hiyo ni dhidi ya Mbeya City, Juni 24 huku mingine ikiwa ya Julai ambayo ni dhidi ya Tanzania Prisons, Julai mosi na Ndanda, Julai 5 kama akifunguliwa mipaka ya Sudan baada ya kumalizika kwa marufuku iliyopo nchini humo, Juni 29, ina maana anaweza kurejea mwanzoni mwa Julai.

Hivyo, haitokuwa rahisi kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Sudan itaanza mchakato wa kuwarudisha wahamiaji waliyokuwa wamepotea kupitia ndege na njia za kuvuka mpaka kuanzia Jumapili.

SOMA NA HII  SADIO MANE NI BALAA TUPU NDANI YA LIGI KUU ENGLAND