Home Habari za michezo PAMOJA NA KUAMRIWA KURUDI YANGA…FEI TOTO AIGOMEA TFF…WAKILI WAKE KAANIKA A-Z….

PAMOJA NA KUAMRIWA KURUDI YANGA…FEI TOTO AIGOMEA TFF…WAKILI WAKE KAANIKA A-Z….

Habari za Yanga

Wakati mbivu na mbichi ya sakata la Yanga na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ ikitarajiwa kujulikana leo wakati Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) itatoa hukumu ya shauri hilo, upande wa mchezaji huo umegoma mchezaji huyo kurudi Jangwani.

TFF ilitoa taarifa kwamba Fei ni mchezaji wa Yanga kimkataba, ila taarifa rasmi ingetolewa jana, ila upande wa kiungo huyo umeweka bayana kwamba hawakubaliani na hilo na wataenda CAS.

Mwanasheria Nduruma Majembe anayemsimamia Fei alikiri kupokea barua ya TFF iliyothibitisha kiungo huyo kuwa bado ni mchezaji wa Yanga, lakini aliweka wazi hawajaridhishwa na maamuzi hayo na wanajipanga kwenda mbele zaidi.

“Sidhani kama haki imetendeka, tumejipanga kuendelea kutafuta haki, kufika Jumatatu tutakuwa tumejua nini tufanye kati ya kuomba review (mapitio) au tunaenda mbele zaidi hadi CAS ili kuhakikisha haki inatendeka,” alisema Majembe ambaye pia alisimamia kesi ya Benard Morrison dhidi ya Yanga mwaka juzi na kushinda.

Kwa upande wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kupitia, Mwenyekiti Said Sudi imeeleza kuwa huru na wapo tayari kumpa nafasi ya kukata rufaa Fei na kama atahitaji kwenda mbele zaidi, watamruhusu.

“Tulichokiamua bado kiko vile vile, Feisal ni mali ya Yanga, lakini kama hawajaridhika na maamuzi hayo wana nafasi ya kukata rufaa na kama atataka kwenda CAS sisi hatuna shida,” alisema Sudi.

Taarifa zinadai kuwa Fei hayupo tayari kurudi Yanga na wasimamizi wake wanafanya kila liwezekanalo kwa gharama yeyote ili kiungo huyo awe huru kwani tayari wamemtafutia timu nyingine ya kucheza mabayo hadi sasa haijawekwa wazi licha ya kuhusishwa na Azam FC.

SOMA NA HII  TIKETI MECHI YA YOUNG AFRICAN(YANGA) VS US MONASTIR...FULL HOUSE FULL SHANGWE...MWANANCHI UPO TAYARI?