Home Habari za michezo PAMOJA NA KUFUNGWA….RONALDO AMFANYIA KITU MBAYA MESSI UWANJANI…

PAMOJA NA KUFUNGWA….RONALDO AMFANYIA KITU MBAYA MESSI UWANJANI…

Ronaldo and Messi Yesterday

Mchezo wa kirafiki kati ya PSG dhidi ya kombaini ya mastaa wa Al Hilal na Al Nassr umemalizika mjini Riyadh nchini Saudi Arabia ambapo PSG amefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 5-4.

Mchezo huo uliowakutanisha miamba wawili wa soka duniani, Lionel Messi wa PSG na Ronaldo wa Al Nassr ulisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ulimwenguni kote.

Katika mchezo huo, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufunga magoli mawili (moja la penati dakika ya 34 na jingine dakika ya 45+6′) huku Messi akifunga goli moja tu ambalo aliliweka kimyani mapema kabisa dakika ya 3 tu ya mchezo.

Mchezo umemalizika kwa PSG kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya combine ya Al Hilal na Al Nassr.

Wengine waliofunga kwa upande wa Al Hilal na Al Nassr ni Hyun-Son dakika ya 56 na Talisca dakika ya 90+4′ ambapo kwa upande wa PSG ni Marquinhos dakika ya 43, beki Sergio Ramos dakika ya 53, Kylian Mbappe dakika ya 60 kwa penati na Ekitike dakika ya 78.

SOMA NA HII  HUU HAPA MCHEZO MPYA KWENYE KASINO BOMBA YA MERIDINAIBET..USHINDI NI MTELEZO SANA..