Home Uncategorized MAJEMBE MANNE YA KAZI YAANDALIWA KUZIBA PENGO LA LAMINE

MAJEMBE MANNE YA KAZI YAANDALIWA KUZIBA PENGO LA LAMINE


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, raia wa Ubelgiji, amefunguka kuwa hakutakuwa na pengo lolote la kumkosa beki wake wa kati Lamine Moro kwenye mechi atakazokuwa nje kwa sababu ana zaidi ya wachezaji wawili wa kuziba nafasi hiyo.
Kocha huyo ameongeza kwamba tayari ameshawaandaa Kelvin Yondani, Andrew Vincent,’Dante’ na Ally Mtoni, ‘Sonso’ kwa ajili ya kuziba nafasi ya beki huyo Mghana.
Lamine amefungiwa kucheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara na kamati ya utendaji kutokana na kosa la kumrukia kwa makusudi na kumpiga teke kiungo wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto ambaye naye amefungiwa mechi tatu.

Eymael amesema kuwa hakutakuwa na pengo la Lamine hata kidogo kwa sababu wachezaji hao wawili ambao ni pamoja na Ally Mtoni ‘Sonso’  na Kelvini Yondani wanaweza kutumika katika nafasi hiyo na kucheza vizuri.
“Kwanza kuhusu Lamine ni mchezaji mzuri na ambaye nimemtumia sana kwenye mechi zetu lakini naona kukosekana kwake wala haitakuwa tatizo kubwa.
“Nasema hivyo kwa sababu Yondani amekuwa kwenye fomu ya hali ya juu, kwa hiyo anaweza kucheza na Makapu (Said) na wakawa na muunganiko mzuri tu kwenye mechi zote ambazo tutamkosa.
“Lakini pia namrudisha Sonso (Ally Mtoni) katika kundi na ana uwezo wa kucheza hapo, pia usisahau kuhusiana na Dante ambaye naweza kumtumia pia. Kwa hiyo utaona kwa kiwango gani hakutakuwa na madhara ya kumkosa,” alisema Eymael.
SOMA NA HII  STAA HUYU WA SIMBA ANAJUTA KUONDOKA YANGA, STORI KAMILI IKO HIVI