Home news SOKA LA BONGO ONLINE MEDIA SALAMU ZA MWAKA MPYA…SOMA YOTE INAKUHUSU…

SOKA LA BONGO ONLINE MEDIA SALAMU ZA MWAKA MPYA…SOMA YOTE INAKUHUSU…

Soka la Bongo Online Media 2023

Menejementi ya Soka la Bongo Online Media, inakutakia kheri na baraka kwa mwaka 2023, tunashukuru kwa kuwa nasi kwa mwaka 2022, hivyo tunaomba uendelee kuwa nasi kwa mwaka huu wa 2023.

Soka la Bongo bado inaendelea kuamini na kusimamia kwenye ukweli na uwazi, hivyo kwa mwaka huu wa 2023, tunakuhaidi kuendelea kukuhabarisha na kukuburudisha kwa viwango vywa juu zaidi.

Kwa mwaka 2023, Soka la Bongo Online Media, tunakusudia kufanya matukio mengi zaidi ya kijamii ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kidogo tunachopata.

Mbali na hivyo, Mwaka huu wa 2023, tunakusudia kuwa na tuzo maalumu kwa ajili ya wapenzi wa soka la bongo, ambapo taarifa kamili itatolewa na menejimenti pindi na wakati utakapiwadia.

Aidha katika kuunga mkono Serikali katika kupambana na uhaba wa ajira, Soka la Bongo Online Media tumejipanga kwa mwaka huu kutoa nafasi ya ajira kwa vijana wa kitanzania wenye sifa na uwezo kwenyeΒ  nafasi mbalimbali .

Kipekee Soka la Bongo, tunaamini tupo hapa kwa ajili yako, hivyo tunakila sababu ya kuhakikisha unakuwa wa kwanza kwenye kila jambo lihusulo michezo.

Hivyo, Kwa mwaka 2023 tunatazamia kuzindua App yetu ambapo itakusogeza karibu zaidi na matukio yote ya kimichezo ndani na nnje ya nchi bila kusahau kufuatilia mechi mubasahara.

Katika kuufanya mwaka huu unakuwa wa kipekee zaidi kwako, Tumepanga mwaka huu kuzindua TV yetu ya mtandaoni, ambapo itaenda sambamba na jarida la michezo, hii yote ni katika kuhakikisha tunakidhi kiu yako ya kuhabarika.

Tunatambua kibinadamu pengine mwaka 2022, kuna mahali tuliteleza na kwenda nnje ya matarajio yako, tafadhali usisite kuwasiliana nasi na kutueleza ili tuboreshe na kuzidi kukuhudumia kwa viwango na matarajio yale yale uliyoyakusudia.

Kipekee tunaendela kutoa pongezi zetu za dhati kwako kwa kuwa miongoni mwa mamilioni ya wasomaji wetu ambao umefanikiwa kuuona mwaka 2023, hivyo Mungu akubariki na kuzidi kukuimarisha mara dufu.

Mwisho na kwa umuhimu, tunapenda kutoa shukrani zetu pia kwa wadau wetu wa kibiashara ambao wamekuwa pamoja nasi kwa mwaka 2022, kwa kuwataja ni pamoja na (Meridianbet, M-Bet, Sokabet, Infinix, Tecno, CRDB Bank, Serengeti Lager , ) na wengine wengi ambao wamechagua kufanya kazi na sisi.

Tunawahaidi kuendelea kutoa huduma bora yenye viwango tarajiwa katika kuyafikia malengo yenu.

Pia tunatoa wito kwa makampuni mengine zaidi kujumika nasi na kuwa sehemu ya wanafamilia zaidi ya Milioni 100 wanaotufuatilia kila kona ya dunia yetu.

Tunawatakia kheri, baraka na fanaka kwa mwaka 2023, ukawe ni mwaka wa rehema na neema kwako, ukawe ni mwaka wa shibe ya furaha na amani kwenye maisha yako.

Happy New Years…..

SOMA NA HII  ALICHOSEMA ALLY MAYAYI KUHUSU SHABAN DJUMA...ADAI SI KILA MCHEZAJI ANAUWEZO...