Home Habari za michezo KABURU AIKALIA SIMBA SC KOONI…TFF WAIBUKA NA KUTULIZA HALI…

KABURU AIKALIA SIMBA SC KOONI…TFF WAIBUKA NA KUTULIZA HALI…

Habari za simba

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi mkuu wa Simba SC, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, aliyekatwa jina lake ameliamsha baada ya kuiburuza Kamati ya Uchaguzi wa klabu hiyo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akikata rufaa dhidi ya uamuzi aliofanyiwa.

Uchaguzi wa Simba SC umepangwa kufanyika Januari 29 mwakani na Kaburu hajakubaliana na uamuzi wa kukatwa kwa jina lake na kukimbilia TFF kuitafuta haki wakati mchakato wa uchaguzi huo ukiendelea.

Mapema Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC iliwaondoa wagombea mbalimbali wa mchakato huo wa uchaguzi akiwamo Kaburu katika mchujo wa awali na kubakisha wagombea 14 wakiwamo wawili wanaowania uenyekiti na 12 wa Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya TFF zinasema kwamba Kaburu aliukatia rufaa uamuzi huo akiwa na hoja mbili kubwa akianza na uhalali wa kamati hiyo akidai haikuwa na sifa za kuendesha uchaguzi huo.

Hoja ya pili ya Kaburu ni kwamba ameeleza jinsi Kamati ya Uchaguzi ilivyomnyima haki yake kwa kutompa taarifa ya kwanini jina lake limeondolewa katika mchujo huo kitu ambacho anaamini hakikuwa halali.

Tayari rufaa hiyo imeshasikilizwa juzi katika makao makuu ya TFF na  kwamba wakati wowote uamuzi wa rufaa hizo utatolewa.

“Tumeshasikiliza hiyo rufaa ya Kaburu, subirini tu wakati wowote mtapewa majibu,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati iliyosikiliza rufaa hiyo.

SOMA NA HII  EHEE..PAMOJA NA KUWA BENCHI MSIMU MZIMA...ABDALLAH SHAIBU 'NINJA' ASINYA KATABA JIPYA YANGA...SABABU NI HII TU...