Home Habari za michezo TP MAZEMBE WAMNYIMA RAHA NABI….AFUNGUKA A-Z JINSI WANAVYOMKONDESHA…

TP MAZEMBE WAMNYIMA RAHA NABI….AFUNGUKA A-Z JINSI WANAVYOMKONDESHA…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi, amefichua kuwa, licha ya ushiriki wao katika Kombe la Mapinduzi, lakini mipango na mikakati yake mikubwa ipo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa kuwa wanataka kufanya makubwa.

Nabi ametoa kauli hiyo kabla Yanga SC kucheza mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi Kundi B dhidi ya KMKM, jana Jumatano.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, Yanga SC imepangwa Kundi D na timu za US Monastir ya Tunisia, Real Bamako (Mali) na TP Mazembe (DR Congo).

Kocha huyo amesema kwamba: “Hatuna sababu ya kupuuza wala kukwepa kwa sababu ni mashindano ambayo yapo karibu kila mwaka na lazima tushiriki kwa ajili ya kutafuta ubingwa kama ilivyokuwa katika misimu mengine kwa sababu ni heshima kwetu kuchukua ubingwa wa michuano hii.

“Lakini binafsi nimekuwa nikiangalia zaidi Kombe la Shirikisho Afrika kwa sababu tunahitaji kufanya vizuri na kufika katika hatua kubwa kutokana na wapinzani ambao tutakutana nao, ukiangalia TP Mazembe, Real Bamako na hata Monastir wote siyo wa kupuuza.”

SOMA NA HII  KAPOMBE ATULIZA MZUKA SIMBA...AFUNGUKA WALICHOFANYIWA NA BENCHIKHA....