Home Habari za michezo YANGA WATOA TAMKO HILI KUHUSU SHABIKI ALIYESHAMBULIWA KWA MKAPA

YANGA WATOA TAMKO HILI KUHUSU SHABIKI ALIYESHAMBULIWA KWA MKAPA

Habari za Yanga SC

Kupitia mitandao ya kijamii kumesambaa video ikionyesha shabiki aliyevaa jezi ya Yanga akishambuliwa na mashabiki waliovalia jezi za Simba katika Uwanja wa Mkapa.

Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick ameandika kupitia akaunti yake kuwa kesho Oktoba 30 klabu hiyo itawasilisha malalamiko yake na kuomba hatua kali zichukuliwe.

“Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisaa, hakuna sababu ya msingi ya kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni watani wa jadi sio maadui,”

Ameongeza; “Naiomba Bodi ya Ligi Kuu, Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jeshi la Polisi wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe,”

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAKOSA WAARABU...BOCCO ASHUSHA 'PRESHA' SIMBA..DAKTARI AFUNGUKA A-Z...