Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA HOROYA…MANULA ‘ACHANWA LIVE’ KUHUSU UDHAIFU WAKE…

KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA HOROYA…MANULA ‘ACHANWA LIVE’ KUHUSU UDHAIFU WAKE…

Habari za Simba leo

KIPA wa zamani wa Simba, Kelvin Mhagama amekitaka kikosi cha Simba kuwa makini kwenye michuano ya kimataifa, huku akimpa ujanja kipa Aishi Manula akitaka awe macho kwenye ishu za mipira ya faulo.

Simba inatarajiwa kushuka ugenini kesho kucheza dhidi ya AC Horoya katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa nchini Guinea.

Katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu, Manula alifungwa bao la friikikii na kiungo wa Singida Big Stars, Bruno Gomes, kitu kilichomfanya Mhagama kumkumbusha kipa huyo kuongeza umakini kwenye mipira ya friikiki.

Mhagama ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Simba mwaka 2003 kilichoitoa Zamalek na kupata nafasi ya kushiriki makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika alisema kocha wa makipa wa Zakaria Chlouha anatakiwa kumuongezea mbinu za kupanga ukuta Manula.

“Kidogo ana shida katika faulo anashindwa kupiga hesabu kati ya ukuta na position akae wapi kulingana na upande mpira unapokuwa.

“Anatakiwa kuupanga ukuta vizuri kwa kuweka mwanzo na mwisho wa ukuta wachezaji warefu, aruke kwa haraka kwa sababu mipira mingi inapigwa juu.

“Ile mipira huwa haidakwi bali inapewa lifti na huwa mara nyingi inakuwa kona,sasa hili ni muhimu kwa Simba katika mashindano ya kimataifa kosa moja la kipa linaharibu mchezo mzima.

“Ila lazima tukubali bado Manula anaendelea kuwa kipa bora mwenye uwezo na kumpata kama yeye kwa sasa hivi ni kazi kwani ametengenezwa kwa muda mrefu,”alisema Mgahama ambaye amewahi kuizea timu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda.

Kuhusu Simba kwenye michuano ya kimataifa alisema; “Simba inayocheza mashindano ya kimataifa ni tofauti kabisa na ile inayocheza ligi ,Simba imebadilika sana katika siku za hivi karibuni angalia mchezo wa mwisho dhidi ya Al Hilal walicheza vizuri,” alisema.

SOMA NA HII  TULIKAA KINYONGE SANA...MUDA WA KUFURAHI NA KUNUNA UMERUDI...LIGI KUU YA MOTO