Home Habari za michezo BAADA YA KUFUNGWA JUZI…REFA WA KIMATAIFA AWAPA SIMBA MBINU HIZI ZA KUTINGA...

BAADA YA KUFUNGWA JUZI…REFA WA KIMATAIFA AWAPA SIMBA MBINU HIZI ZA KUTINGA ROBO…

Habari za Simba

Mwamuzi mwandamizi wa soka nchini Tanzania, Osman Kazi amewapa mbinu Timu ya Simba ili waweze kutoboa hatua ya Makundi na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Mabingwa Afrika.

Kazi amesema hayo jana wakati akihojiwa na wanahabari kutoa tathmini yake mara baada ya mchezo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kumalizika huku Yanga akiibuka na ushindi mnono wa bao 3-1 dhidi ya Mazembe.

Kauli hiyo ya Kazi inakuja kufuatia kichapo walichokipata Simba katika mechi zao mbili za mwanzo za kundi C katika michuano hiyo ambapo Simba alifungwa na Horoya bao 1-0 na mechi ya pili akafungwa tena nyumbani na Raja Casablanca.

“Simba mechi ya kwanza wamecheza ugenini, waliupiga mwingi sana kule lakini bahati haikuwa yao na hawakupata bao. Wamekuja hapa wamecheza na Raja Casablanca, moja ya vilabu bora sana barani Afrika.

“Nilijua kabisa mechi ya Raja itakuwa kipimo kikubwa sana kwa Simba, sababu kiwango cha Raja ni kikubwa sana, pira walikuwa hawaukimbizi bala wanakaa kwenye njia na mpira unawafuata wao.

“Sitaki kuwa mtabiri lakini naiona Raja ikipata pointi zote 18 kwenye kundi lao. Simba wajipange, wanakwenda kucheza dhidi ya Vipers, wahakikishe lazima wanachukua alama tatu, wakirudi hapa na Vipers washinde, Horoya akija hapa wamalize mahesabu yao.

“Simba kuvuka hatua ya makundi sio kama kuna shida, na tusiwashushe sana kwa kiwango chao dhidi ya Raja, wamepatwa na kitu kizito kutoka klabu nzito,” amesema Osman Kazi.

SOMA NA HII  CAF WALIVYOIPELEKA 'DABI' YA SIMBA NA YANGA ALGERIA...SHOW NZIMA ITAKUWA HIVI...