Home Habari za michezo ACHANA NA YANGA KUUPIGA MWINGI DHIDI YA WATUNISIA..ILA KAMA SIO LOMALISA NA...

ACHANA NA YANGA KUUPIGA MWINGI DHIDI YA WATUNISIA..ILA KAMA SIO LOMALISA NA FARIDI WANGEUMBUKA..

Yanga Tunisia Jana

Wawakilishi wa Tanzania Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga juzi Jumapili walipoteza mechi ya kwanza ugenini hatua ya makundi dhidi ya US Monastir baada ya kufungwa mabao 2-0, Tunisia katika Uwanja wa Olympique de Rades.

Mabao ya Monastir yalifungwa na Mohamed Saghroui dakika 10, kwa kichwa akimalizia mpira wa faulo uliochongwa na Haykeul Chikhaoui na Boubacar Traore alifunga bao la pili dakika 15, akiunganisha kwa kichwa kona ya Chikhaoui.

Baada ya kufungwa mabao mawili uchezaji ulibadilika kwa Monastir hawashambulia mara kwa mara na hata wachezaji wa Yanga waliongeza umakini kwenye mashambulizi machache yaliyofanywa hayakuwa ya hatarini kama dakika 15 za mwanzo wa mchezo.

Takwimu hadi mechi inamalizika Yanga ilipiga jumla ya mashuti saba huku matatu yakilenga lango, wakati Monastir ilipiga manane na sita yamelenga lango, umiliki wa mpira Yanga ilikuwa asilimia 59 wenyeji asilimia 41.

MIPIRA YA KROSI

Miongoni mwa silaha kwa timu za Afrika zilizokuwa na asili ya nchi za Kiarabu kama Misri, Tunisia, Algeria na nyingine wakati wa kushambulia hutumia vyema mipira iliyokufa kama kona na faulo kuwa mabao.

Yanga ilitakiwa kuingia kwa tahadhari kubwa kuhusiana na hilo ila bahati mbaya ilishindwa kung’amua mtego huo mapema kwani hadi dakika 15, ilikuwa imeruhusu mabao mawili yaliyozalishwa kutokana na kona na faulo.

Bao la kwanza alilolifunga Saghroui lilitokana na wachezaji watatu wa Yanga, Dickson Job mpira wa juu ulimvuka kutokana na kimo chake wakati, Khalid Aucho na Yannick Bangala wote walishindwa kumzuia mfungaji.

Traore aliyefunga bao la pili aliruka nyuma ya Bangala mbele ya Djuma Shabani wote mabeki wawili wa Yanga walifanya uzembe na kushindwa kumzuia.

UBORA WA DIARRA

Pengine kama si ubora wa kipa, Djigui Diarra Yanga ingeruhusu zaidi ya mabao mawili kwani aliokoa mara zaidi ya mbili pale wachezaji wa Monastir walivyotengeneza nafasi za kufunga mabao.

Nafasi mbili za Traore na moja Youssouf Oumarou uso kwa uso na Diarra kama si ubora wake, Monastiri ingepata ushindi mnene zaidi kwenye mchezo huo wa kwanza.

Ubora wa Diarra uliendelea kuiweka Yanga sehemu salama kwani amekuwa na muendelezo mazuri ya kuonyesha kiwango bora hasa timu hiyo inaposhambuliwa.

BAADA YA KUPATA BAO

Monastir baada ya kupata mabao mawili ya mapema pengine labda malengo yao yalitimia, hawakushambulia kwa haraka na kulisakama lango la Yanga kama walipokuwa hawajapata bao.

Pengine ulikuwa mpango wao kufunga mapema na baada ya hapo kulinda ushindi na hakupoteza mipira mara kwa mara. Monastir haikushambulia kwa haraka tena ilicheza mipira mifupi na pasi nyingi eneo la kati mwa kiwanja. Yanga nayo ilibadilika kwani utulivu uliongezeka.

Yanga baada ya kufungwa mabao ya mapema utulivu uliongezeka kwa upande wao pamoja na kufanyiwa mashambulizi machache ikiwemo yale ya krosi na kona haikufanya makosa tena ya kuruhusu mabao.

HUDUMA KWA MAYELE

Miongoni mwa changamoto Yanga iliyokutana nayo ni mshambuliaji wake Fiston Mayele kushindwa kufunga labda kwa kutopatiwa huduma sahihi.

Hadi mechi inamalizika Mayele alihusika kwenye mashambulizi mawili hatari akipiga shuti moja lililolenga lango na lingine lilikwenda nje kipindi cha pili.

Mayele alishindwa kupata huduma kutokana na ubora wa mabeki wawili wa kati, Ousmane Ouattara na Mohamed Saghraoui kumzuia na kushindwa kuonyesha makali.

ULIZI WA YANGA

Yanga baada ya kuruhusu mabao mawili iliimarika na kuwa bora kwenye eneo la ulinzi kwa kufuta makosa yaliyoleta madhara kama ilivyoruhusu mabao mawili.

Haikuruhusu mipira mingi ya kona, faulo wala krosi za hatari langoni kwao na wachezaji wa Monastir wangeweza kupata mabao licha ya kupata nafasi chache.

Monastir ukiachana na nafasi mbili ilizotumia ilipata nyingine tatu ilizoshindwa kufanya hivyo kutokana na uimara wa wachezaji wa Yanga akiwemo kipa, Diarra aliyeonekana kuwa mkali aakiwataka mabeki wake kukaba kwa usahihi.

MABADILIKO YA MFUMO

Yanga haikuingia kwa kujilinda zaidi kwenye mechi hiyo ilianza na mfumo wao pendwa (4-2-3-1), kazi ilikuwa ngumu wakati wa kufanya mashambulizi kwani hayakuwa na madhara kwa wapinzani wao.

Kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko ya kuingia, Kennedy Musonda, Farid Mussa, Mudathir Yahya na Joyce Lomalisa Yanga ilionekana kubadilika kwenye uchezaji na kuanza kufanya mashambulizi.

Musonda na Aucho kila mmoja alimtengenezea nafasi moja ya kufunga mshambuliaji Mayele katika kipindi cha pili lakini zote alishindwa kuzitumia.

Nafasi moja alipiga shuti na kipa wa Monastir, Ben Said alilizuia na shuti lingine liilitoka nje. Kuna uwezekano mkubwa mabeki wa Monastir walipata nafasi ya kuisoma Yanga na kuijua mikimbio ya Mayele.

SOMA NA HII  KUHUSU UBINGWA WA YANGA MSIMU HUU...BARBARA AIBUKA NA KUTOA KAULI HII MOJA TU...AMTAMBUA NABI....