Home Habari za michezo AHMED ALLY: TUWE WA KWELI…WACHEZJI WENGI WA SIMBA WAMECHOKA MNOO..HAWAWEZI TENA…

AHMED ALLY: TUWE WA KWELI…WACHEZJI WENGI WA SIMBA WAMECHOKA MNOO..HAWAWEZI TENA…

Habari za Simba

Klabu ya Simba imekiri kupungua kwa ubora wa baadhi ya wachezaji wake kutokana na kucheza michuano ya kimataifa na Ligi Kuu kwa muda mrefu bila kupumzika.

Meneja Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, Ahmed Ally, amesema kuna baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wamefanya kazi kubwa kwa miaka mitano mfululizo kwenye michuano ya kimataifa, Ligi Kuu na michuano mingine, hivyo kama binadamu hawawezi kuwa na uwezo, kiwango au ubora ule ule waliokuwa nao awali.

“Simba ipungua ubora kidogo, lazima tuwe wa kweli. Kwanza kuna nyota wetu ambao ubora wao umepungua kidogo kwa sababu ya kuchoka, wamefanya kazi kubwa kwa miaka mitano, wamecheza sana kwa miaka yote hiyo michuano ya kimataifa, Ligi Kuu na michuano mingine mfululizo.

“Hakuna binadamu ambaye anaweza kukupa asilimia 100 kwa miaka mitano, Mungu hajamuumba binadamu wa hivyo. Na unafahamu mpira kazi ya nguvu na kutumia akili na muda, unapocheza inatakiwa akili yako ifanye kazi kwa haraka sana, ukifanya kazi hiyo kwa miaka hiyo mfululizo lazima utachoka na kiwango kinapungua, ndiyo maana unaona ubora huo umepungua kwa sasa,” alisema Ahmed.

Akatoa mfano mchezaji kama Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, ambaye anacheza hatua ya awali ya michuano ya kimataifa, hatua ya kwanza, mechi sita za makundi na robo fainali kwa miaka mitatu, haiwezekani baada ya hapo atakuwa kwenye kiwango kile kile, ni lazima kitapungua kidogo.

Mbali na hilo alisema wapo baadhi ya wachezaji ambao walikuwa bora, lakini wameondoka kwenye klabu hiyo kwa kuuzwa.

“Kingine ambacho unaweza kuona ubora huo umepungua kidogo kwenye timu yetu, wapo watu wameondoka kwenye timu yetu, ama wameuzwa, au viwango vyao vilipungua, wakauzwa.

Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, anacheza hatua ya awali ya michuano ya kimataifa, hatua ya kwanza, mechi sita za makundi na robo fainali kwa miaka mitatu, usitegenee baada ya hapo atakuwa kwenye kiwango kile kile, ni lazima kiwango kitapungua kidogo.

Hata hivyo, baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba wamegawanyika kuhusu timu yao ambayo Jumamosi iliyopita ilichapwa mabao 3-0 dhidi ya Raja Casablanca, mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Baadhi wanamlaumu Kocha Mkuu, Robert Oliveira kuwa upangaji wake usio sahihi na mfumo wake mgumu ndiyo uliosababisha kipigo hicho, wengine wakidai kuwa aina ya wachezaji wengi waliopo kwenye kikosi umri wao ni mkubwa.

Hivyo kutoweza kuendana na falsafa ya kocha, na wapo walioenda mbali zaidi waliodai karibuni nusu nzima ya wachezaji hawana viwango vya kuichezea timu hiyo, hivyo kikosi kinahitajika kisukwe upya msimu ujao.

SOMA NA HII  MKWANJA WAKO UPO KWENYE LIGI KUU INDIA, TAZAMA ODDS ZA USHINDI!