Home Uncategorized BREAKING: MUUAJI WA SIMBA AREJESHA MKATABA YANGA, SASA UHAKIKA

BREAKING: MUUAJI WA SIMBA AREJESHA MKATABA YANGA, SASA UHAKIKA

BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amerejesha mkataba wake kwa mabosi wake ambao ni kampuni ya GSM kupitia kwa Mkurugenzi wa uwekezaji Hersi Said baada ya kumalizana nao muda mrefu alipotua ndani ya Yanga.

Morrison alisaini dili hilo la miaka miwili mwezi Februari kabla ya mechi ya Machi 8 dhidi ya Simba Ila hakurudisha mkataba wake kwa mabosi wake.


Kwenye mechi hiyo, Morrison alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 44 lililoipa pointi tatu Yanga, Uwanja wa Taifa.

Hali hiyo imekuja kutokana na kuenea tetesi kwamba ameingia kwenye anga za Simba ambao walikuwa wanaiwinda saini yake

SOMA NA HII  MFAHAMU VIZURI SHIBOUB ALIPOZALIWA MPAKA ANATUA SIMBA - VIDEO