Home Habari za michezo KATIKA MASTAA WOOTE WA AL AHLY….HUYU ….YANI HUYUU…AKICHIWA NAFASI TU…SIMBA WAMEISHA…

KATIKA MASTAA WOOTE WA AL AHLY….HUYU ….YANI HUYUU…AKICHIWA NAFASI TU…SIMBA WAMEISHA…

African Football league

Kuelekea mchezo wa leo wa ufunguzi wa African Football League kati ya Simba dhidi ya Al Ahly utakaopigwa saa 18:00 Jioni katika dimba la Benjamin Mkapa, nakusogezea takwimu za wachezaji ambao wanapaswa kuchungwa zaidi na wachezaji wa Simba hii leo.

Tangu msimu wa Ligi kuu nchini Misri umeanza klabu ya Al Ahly imecheza michezo miwili (2) na imeshinda michezo yote miwili (2), ipo nafasi ya tano (5) ya msimamo wa Ligi ikiwa na alama sita (6), katika michezo hiyo miwili imefunga jumla ya magoli saba (7) na kuruhusu goli moja (1) pekee.

Mchezaji wa kuchungwa zaidi hii leo ndani ya klabu ya Al Ahly ni Percy Tau raia wa Afrika Kusini ambaye hadi hivi sasa ndiye kinara wa upachikaji magoli ndani ya klabu hiyo akifunga magoli manne (4) na kinara wa utengenezaji wa magoli ndani ya kikosi hicho ni Emam Ashour ambaye ametoa pasi mbili (2).

Klabu ya Al Ahly pia wamefanya usajili wa nyota kadhaa msimu huu ambao hawajapata nafasi ya kutumika, inawezekana leo wakawa sehemu ya kikosi chao hivyo basi nyota wa zamani wa FC Cologne na Borussia Dortmund, Antony Modeste anapaswa kuchungwa zaidi iwapo ataanza hii leo sambamba na Percy Tau.

Msimu huu Al Ahly imecheza jumla ya michezo mitatu, ya Ligi miwili na FA mmoja, katika michezo yote hiyo imeshinda kuanzia magoli matatu (3) na kuendelea.

SOMA NA HII  DEMBELE KUPEWA DILI JIPYA BARCELONA