Home Uncategorized TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND ZAPEWA ONYO ISHU YA KANUNI ZA AFYA

TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND ZAPEWA ONYO ISHU YA KANUNI ZA AFYA


SERIKALI ya Uingereza, imetoa onyo kwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu England kwa muendelezo wa makosa ya kutojali kanuni ya afya ya kukaa umbali wa mita moja wakiwa kwenye muendelezo wa mechi zao kwa sasa.

Baada ya Ligi Kuu England kuendelea kuanzia Juni 17 kulikuwa na mpango wa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona jambo ambalo limekuwa halifuatwi.

Muda ambao umekuwa ni mgumu kusimamia kanuni hiyo kwa makocha na wachezaji ni wakati wa kushangilia pindi timu inapofunga bao na muda wa kunywa maji.

Ripoti zinaeleza kuwa tayari Serikali imefanya mawasiliano na timu zote kwa kuwaandikia barua juu ya kuwakumbusha kutopuuzia kanuni za afya kwani janga la Virusi vya Corona bado lipo.

Timu 20 zimeandikiwa barua kupewa onyo kwa kuwataka wabadili mienendo yao katika mechi ambazo zimebaki ndani ya Ligi Kuu England kwa sasa.


SOMA NA HII  SIMBA YANGANA MUELEKEO MPYA LIGI YA MABINGWA