Home Uncategorized SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KWA YANGA

SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KWA YANGA


JOHN Bocco, nahodha wa Simba ametuma salamu kwa wapinzani wao Yanga katika mchezo wa kesho, Julai 12 kwa kusema kuwa, wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, sasa wanaangalia Kombe la FA.
Simba imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikiwa imefikisha pointi 81 katika mechi 34 wakibakiwa na mechi nne ambapo hakuna timu itakayofikia pointi hizo huku wakiwa tayari wameshakabidhiwa kombe lao jumla kwa mujibu wa kanuni.

 Katika mechi dhidi ya Namungo FC, Julai 8 Simba ililazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Majaliwa.

Simba imeshinda michezo 25 kati ya 34 waliyocheza, sare sita huku wakipoteza jumla ya michezo mitatu ndani ya ligi.
Bocco amesema kuwa, wanashukuru Mungu kuona wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa kushirikiana na wachezaji na viongozi na kudai kuwa kazi iliyobakia ni kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa Kombe la FA kwa kumtwanga Yanga kisha kufikia hatua ya fainali.

Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa kujituma pamoja na uongozi wetu ambao ndiyo uliofanikisha sisi kufika hapa na kutwaa ubingwa huu.
“Kila mchezaji aliwajibika ipasavyo katika nafasi yake kwa juhudi zote na kuweza kufikia malengo haya, tunachokiangalia hivi sasa ni kuona tunafanikiwa kutwaa Kombe la FA, kikosi chetu kipo vizuri kuelekea mchezo wa Jumapili,” amesema Bocco.
SOMA NA HII  KOCHA HUYU YANGA ANASUBIRI TIKETI ATUE BONGO