Home Habari za michezo SIMBA YANGANA MUELEKEO MPYA LIGI YA MABINGWA

SIMBA YANGANA MUELEKEO MPYA LIGI YA MABINGWA

SIMBA NA YANGA WAOGELEA BAHARI YA MINOTI...MAMA AWALAMBISHA TENDE...WACHEZAJI HAWAAMINI MASIKIO YAO

Upepo umebadilika, vigogo Simba na Yanga sasa wana nguvu ya kupambana kutafuta tiketi ya kucheza robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ambayo baadhi ya makocha nchini wanataja mambo matano wanayoamini yatatoa muelekeo mpya kwa timu hizo kufika hatua hiyo.

Simba na Yanga kila moja ni ya pili kwenye msimamo wa kundi lake, zote zikiwa na pointi tano baada ya ushindi wa mechi zao za Jumanne na Jumatano iliyopita zikicheza nyumbani kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Simba ndiyo ilianza kufufua matumaini Jumanne iliyopita kwa kuichapa Wydad mabao 2-0 na kufikisha pointi tano kwenye kundi B ikitoka mkiani na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye kundi linaloongozwa na ASEC (10) Jwaneng Galaxy yenye pointi nne iko nafasi ya tatu na Wydad inakamata mkia na pointi tatu.

Vivyo hivyo kwa Yanga ambayo Jumatano iliyopita iliifunga Medeama ya Ghana mabao 3-0 na kufikisha pointi tano zilizoipandisha hadi nafasi ya pili kwenye kundi D linaloongozwa na Al Ahly yenye pointi tano lakini ikiwa na mchzeo mmoja wa kiporo dhidi ya CR Belouizdad inayokamata nafasi ya tatu na pointi nne na Medeama ni ya mwisho ikiwa na pointi tatu

Yanga sasa inasubiri kumalizia ngwe yake ya mwisho ya makundi na wababe Al Ahly ugenini na Belouizdad nyumbani, wakati Simba itacheza na ASEC ugenini na Jwaneng Galaxy nyumbani mechi zitakazopigwa mwakani kuanzia Februari zikitakiwa kushinda ili kumaliza makundi na pointi 11 ambazo zitawapeleka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tayari makocha, Abdelhak Benchikha (Simba) na Miguel Gamondi (Yanga) wameeleza mikakati yao baada ya mechi zao zilizopita, Benchikha akisisitiza kuwekeza nguvu zaidi ili kufika robo fainali.

Gamondi yeye alisema, lengo bado halijatimia na ushindi wa juzi ndiyo mwanzo tu wa wao kupambana ili kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo wakifanikiwa itakuwa ni mara ya kwanza Yanga kufika hatua hiyo.

Wakati kila upande ukipiga hesabu za robo fainali, baadhi ya makocha nchini wamesema inawezekana timu zote mbili kufika hatua hiyo, wakitaja mambo matano ambayo yanaweza kuzipa wepesi timu hizo kufika hatua hiyo.

Kocha Adolph Rishard alisema, kikubwa kitakachozipa mwanga wa kufuzu robo fainali timu hizo ni kuendeleza nidhamu ya mechi kwa kuwaheshimu wapinzani, kuweka mkakati unaotekelezeka na wachezaji kujengwa kisaikolojia kutambua umuhimu wa mechi hizo.

“Timu zetu zote mbili zina nafasi ya kufika robo, hivi zinavyokwenda ndivyo zinazidi kunogesha upinzani na kuzifanya kupambana zaidi, hii ikishinda na nyingine inashinda pia,” alisema Rishard.

Kocha huyo mzawa alisema, mechi zao zilizosalia sio rahisi, zinahitaji timu kujipanga na kuziwekea mikakati madhubuti, kauli sawa na iliyotolewa na beki wa zamani wa Taifa Stars, Fred Felix Minziro.

Minziro ambaye kitaaluma ni kocha alisema, timu hizo ziweke malengo ya ushindi kwenye mechi zao za nyumbani.

“Ugenini hata wakipata droo (sare) sio mbaya, japo focus (malengo) ni ushindi kwenye mechi zilizosalia na hilo linawezekana kwani tayari zimetuthibitisha hilo kwa kucheza na timu ambazo wengi waliamini ni bora zaidi lakini tulizifunga hapa Dar es Salaam,” alisema.

Alisema, hakuna mechi rahisi, na mbinu za mpira ni ngumu, lakini inategemea timu zimejipanga vipi na zinacheza vipi kwenye dakika 90.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIZIDI KUNG'ARA....NTIBAZONKIZA AZIDI KUTAKATA LIGI KUU...AMTIMULIA VUMBO CHAMA NA WENZAKE...