Home Uncategorized ZAHERA ATOA MASHARTI MAKALI YA USAJILI YANGA

ZAHERA ATOA MASHARTI MAKALI YA USAJILI YANGA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera ametoa masharti ya usajili wa wachezaji wapya.

Yanga hadi hivi sasa imekamilisha usajili wa wachezaji saba ambao ni Issa Birigimana ‘Walcott’, Patrick Sibomana (Rwanda), Lamine Moro (Ghana), Maybin Kalengo (Zambia), Farouk Shikhalo (Kenya) na Sadney Urikhob (Namibia) na Abdulaziz Makame (Zanzibar).

Timu hiyo imepanga kufanya usajili mkubwa utakaokuwa na kikosi kipana kwa lengo la kufanya vyema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kutwaa ubingwa wa ligi uliochukuliwa mara mbili mfululizo na watani wao Simba.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Kamati ya Kuhamasisha Uchangiaji ya Yanga, Deo Muta alisema kuwa kocha huyo ameacha maagizo kwa uongozi kuhakikisha usajili wa wachezaji wake wote uwe chini ya miaka 27.

Muta alisema, kocha anahitaji wachezaji wengi vijana watakaoendana na kasi ya ushindani ya ligi na michuano ya kimataifa, hivyo kabla ya mchezaji kusajili ni lazima wazingatie umri.

“Mimi sipo kwenye Kamati ya Usajili ya Yanga, lakini kidogo nikumegee kuwa tumepanga kufanya usajili bora na kisasa wa kikosi kipana kitakachoendana na timu yetu.

“Mimi Katibu wa Kamati ya Hamasa ya Uchangiaji wa Yanga, nathibitisha hilo kutokana na michango tunayoendelea kuifanya ambayo itatupa wachezaji wengi wazuri wenye uwezo mkubwa na kuirejesha anga za kimataifa.

“Katika hilo ndiyo maana kocha ametoa masharti ya umri kwa maana ya kusajili wachezaji waliokuwa chini ya miaka 27 na ninaamini kati ya hao ambao tumewasajili hakuna aliyepita zaidi ya kushuka chini,” alisema Muta.

SOMA NA HII  BUSUNGU AFUNGUKIA USAJILI WAKE YANGA