Home Uncategorized ORODHA KAMILI YA WACHEZAJI AMBAO WAMEMALIZANA NA SIMBA NA WALIPO KWA SASA

ORODHA KAMILI YA WACHEZAJI AMBAO WAMEMALIZANA NA SIMBA NA WALIPO KWA SASA


KWA sasa joto la usajili ndio limepamba moto huku kila timu ikiwa bize kukamiisha usajili wa wachezaji ambao wanawahitaji.

Mpaka sasa tayari mabingwa watetezi Simba wamewatangaza rasmi wachezaji watano ambao wamemalizana nao kila kitu na watawatambulisha rasmi Juni 21 Mwanza.

Hawa hapa ambao wamemalizana na Simba mpaka sasa.

John Bocco, nahodha wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili kwa sasa yupo na timu ya Taifa nchini Misri.

Erasto Nyoni, beki kiraka wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, kwa sasa yupo nchini Misri na timu ya Taifa.

Aishi Manula, Mlinda mlango wa Simba, ameongezewa maka mitatu, kwa sasa yupo nchini Misri.

Jonas Mkude, Kiungo wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, yupo Tanzania kwa sasa.

Beno Kakolanya, Mlinda mlango wa Simba amesajiliwa akiwa huru, yupo Tanzania.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO