Home Uncategorized HIKI NDICHO KILICHOMCHELEWESHA MKUDE KUJIUNGA NA KAMBI YA TIMU YA TAIFA STARS

HIKI NDICHO KILICHOMCHELEWESHA MKUDE KUJIUNGA NA KAMBI YA TIMU YA TAIFA STARS

JONAS Mkude, nyota wa Simba amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya ashindwe kujiunga na timu ya Taifa ni matatizo ya kibinadamu yanayomkabili na siyo suala la utovu wa nidhamu.

Mkude alichelewa kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyokuwa imeweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na michuano ya CHAN iliyotarajiwa kufanyika nchini Cameroon hivi karibuni kabla haijaahirishwa kutokana kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mkude amesema: “Haina maana kwamba mimi ni mtovu wa nidhamu ndio maana ninachelewa kujiunga na timu ya Taifa hapana ninaithamini kazi yangu lakini masuala ya kibinadamu ndiyo ambayo yamekuwa yakinitatiza nishindwe kuwahi kwenye kambi,”.

Kocha Mkuu wa Stars, Ettiene Ndayiragije alisema kuwa hawezi kumzungumzia Mkude kwa kuwa hakuripoti kambini.

SOMA NA HII  MFAHAMU VIZURI MAYBIN KALENGO, MTAMBO MPYA WA MABAO YANGA - VIDEO