Home Habari za michezo ISHU YA YANGA NA MORRISON NI KAA LA MOTO…ATAKOSA MECHI ZOTE HIZI...

ISHU YA YANGA NA MORRISON NI KAA LA MOTO…ATAKOSA MECHI ZOTE HIZI MUHIMU…

Habari za Yanga
[the_ad id="25893"]

Klabu ya Yanga imethibitisha nyota wake, Bernard Morrison atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili baada ya kupata majeraha ya nyonga.

Uwepo wa Morrison kwenye kikosi cha Yanga chini ya Kocha wake Mkuu, Nasreddine Nabi ilikuwa inamfanya kuwa na washambuliaji wengi kwenye eneo hilo la ushambuliaji ambalo linaongozwa na Fiston Mayele mwenye mabao 15.

Kutokana na majeraha hayo nyota huyo atakosa mechi zote za hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika akianza na mchezo wa kwanza dhidi ya US Monastir ya nchini Tunisia utakaopigwa Jumapili hii ya Februari 12.

Nyingine ni dhidi ya TP Mazembe (DR Congo) utakaopigwa Februari 19, Real Bamako (Mali) utakaochezwa Februari 26, kisha kurudiana tena na Real Bamako (Machi 7), Monastir (Machi 19) na kumalizia na TP Mazembe Aprili 2.

Katika michezo ya Ligi Kuu Bara atakayokosa ni dhidi ya KMC (Februari 22), Geita Gold (Machi 12) na Kagera Sugar (Aprili 7).

Itakumbukwa kabla ya nyota huyo kukumbwa na majeraha hayo alitoka kuonywa na klabu yake baada ya kuchelewa kurudi kambini wakati Ligi Kuu iliposimama ili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar.

SOMA NA HII  YANGA KAZI INAENDELEA KWA AJILI YA MSIMU MPYA WA 2021/22

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here