Home Habari za michezo KISA ISHU YA MADAKTARI YANGA KUMUOKOA ABIRIA WA NDEGE…MENEJA WAO AIKOMALIA KINOMA…

KISA ISHU YA MADAKTARI YANGA KUMUOKOA ABIRIA WA NDEGE…MENEJA WAO AIKOMALIA KINOMA…

Habari za Yanga

Unaikumbuka ile stori ya madaktari wa timu ya Yanga walivyomsaidia moja ya abiria aliyepata tatizo la kifaya kwenye ndege angani wakielekea nchini Tunisia katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir?

Sasa taarifa ikufikie kuwa, Meneja wa Idara ya Dijitali wa Yanga, Privaldinho akalikumbushia, lakini mara hii akawanyoshea kidole wapinzani wao jambo hilo jema hawaliongelei tena bali wamekalia kuongea vitu visivyo na tija.

Baada ya malamiko hayo ambayo yanaonekana yaliekezwa kwa baadhi ya wachambuzi wa soka nchini, Wananchi kama Wananchi bwana!

Mapovu yakaanza kuwatoka chaaap! Wengi wakiwa wanamlalamikia kuwa kwa kuliongelea jambo hilo ni kama haitendei haki kazi yake aliyoajirwa nayo.

Katika tukio hilo, jopo la madaktari wa Yanga, likiongozwa na Daktari Moses Etutu waliokoa maisha ya abiria mmoja aliyepata changamoto ya afya ndege ikiwa angani.

Tukio hilo lililotokea ndani ya Shirika la ndege la Emirates juzi, majira ya saa 2 kabla ya kutua nchini Tunisia.

Baada ya mgonjwa huyo kuwa kwenye hali mbaya, wahudumu wa ndege walitangaza kama kwenye ndege kuna mtu yoyote mwenye taaluma ya udaktari asimame kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Hapo ndipo madaktari wa Yanga walisimama na kuwahi kumpa huduma ya kwanza mgonjwa huyo aliyekuwa na changamoto ya sukari na maradhi mengine.

Wakati rubani wa ndege akifikiria kutua uwanja wa ndege wa karibu, Daktari Etutu aliwahi na kutoa huduma na hali ya mgonjwa huyo ikaimarika na ndege kuendelea na safari.

SOMA NA HII  TETESI....MANZOKI KUONEKANA KWENYE SIKU YA WANANCHI YA YANGA....MIPANGO YOTE NI KIMYA KIMYA NAMNA HII...