Home Simba SC GOMES ASISITIZA KUITAKA NAFASI YA YANGA

GOMES ASISITIZA KUITAKA NAFASI YA YANGA


KOCHA mkuu wa Simba Didier Gomes, ametamba kuwa, licha ya kuwaheshimu wapinzani wake katika mchezo wa kesho Tanzania Prisons, lakini anaamini kikosi chake kitaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi  wa mabao 3-0 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya JKT Tanzania.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Prisons Gomes amesema:”Kikosi chetu kiko tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons, tunajua hautakuwa mchezo rahisi kutokana na uhalisia wa timu ambayo tunakwenda kucheza nayo.

“Simba ilipoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya timu hii, na hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi dhidi yao kwani hiyo inaonyesha ni kwa kiasi gani wana timu ambayo inaweza kupambana.

“Lakini matokeo ya ushindi katika mchezo huu ni ya muhimu kwetu, tunapaswa kushinda ili kuendelea kuusogelea zaidi uongozi wa ligi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Yanga,”

SOMA NA HII  ILIBIDI MATAIFA MATATU YAUNGANE KUPATA USHINDI SIMBA