Home Habari za michezo KISA UJIO WA MAZEMBE NA RAJA ….TANZANIA YAANDIKA REKODI HII MPYA AFRIKA…

KISA UJIO WA MAZEMBE NA RAJA ….TANZANIA YAANDIKA REKODI HII MPYA AFRIKA…

Habari za Michezo

Mwaka 2013, Tanzania iligonga vichwa vya habari baada ya kuwakutanisha marais wawili wa Marekani, Barack Obama aliyekuwa madarakani wakati huo na mtangulizi wake, George W. Bush.

Gazeti la New York Times la Marekani liliita kukutana huko kuwa ni an unprecedented chance encounter a world away from home, yaani nafasi ya bahati ya kukutana katika dunia ya mbali na nyumbani ambayo haijawahi kutokea hapo kabla.

Marais wa Marekani kukutana ughaibuni ilikuwa habari kubwa kutokana na historia ya taifa. Japo ilipata uhuru 1776, Marekani ilikuwa nchi ya kujitenga sana.

Marais wa nchi hiyo walikuwa hawasafiri nje ya nchini yao,hadi ilipopita zaidi ya miaka 200 baada ya uhuru.

Rais wa kwanza kuvunja mwiko huu alikuwa Teddy Roosevelt pale mwaka 1906 alipotembelea ujenzi wa mfereji wa Panama.

Mfereji wa Panama ni kama mto wa kutengeneza unaounganisha bahari mbili za Atlantic na Pacific. Kuunganishwa kwa bahari hizi maana yake ilikuwa kuunganisha njia ya maji kati ya Amerika Kusini na Kaskazini.

Kwa hiyo kutoka Rais kutosafiri hadi marais wawili waliofuatana kukutana nje, utaona ilikuwa habari kubwa kiasi gani.

DUNIA ILITIKISIKA!

Takribani miaka 10 baada ya tukio hilo, ardhi ya Tanzania inafanya tena maajabu, lakini safari hii ni kwenye soka, siyo siasa.

Miamba miwili ya soka la Afrika, TP Mazembe ya DRC na Raja AC ya Morocco zimekutana jijini Dar Es Salaam katika mwendelezo uleule ambao New York Times iliuita ‘an unprecedented chance encounter a world away from home’.

Timu hizi ni miamba hasa kwenye kwenye wa soka la Afrika na ndiyo timu pekee za Afrika kuwahi kufanya vizuri zaidi kwenye Klabu Bingwa ya Dunia.

TP Mazembe ilifika fainali mwaka 2010, Raja AC ilifika fainali mwaka 2013 na Al Ahly walishinda nafasi ya mshindi wa tatu mwaka 2020.

Ndani ya Afrika, miamba hawa kwa pamoja wameshinda ligi ya mabingwa mara nane. TP Mazembe mara tano na Raja AC mara tatu.

Miamba hawa kukutana katika nchi moja ya ugenini ni historia kubwa kama marais wa Marekani kukutana ugenini.

Lakini siyo tu kukutana, wamecheza katika uwanja mmoja ndani ya siku mbili za kufuatana. Hii ni historia.

Ni bahati mbaya tu kwamba mpira wa Afrika hauvuki mipaka. Licha ukubwa walionao miamba haya, lakini wakitoka nje ya nchi zao hawana umaarufu mkubwa.

Watu walisubiri timu zao za Kariakoo zicheze ndiyo waende uwanjani.

Hawakuenda kwa sababu ya ukubwa wa Raja AC au TP Mazembe, hapana. Walienda kwa sababu ya mapeni yao kwa timu zao za Kariakoo.

Huwezi kuwahukumu kwa hilo kwa sababu siyo kosa lao, ni kosa la kihistoria kwamba waliotutangalia hawakuvunja mipaka, na sisi tuliopo hatufanyi jitihada za kuvunja mipaka hii.

Lakini ukiacha hayo na kuangalia tukio la timu hizi kukutana, hii inabaki kuwa moja ya wikendi kubwa zaidi kisoka hapa nchini.

Historia imeandikwa.

SOMA NA HII  IBENGE AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YA CHAMA NCHINI MOROCCO..ATAJA SABABU ZA KUMPIGA BENCHI...