Home Habari za michezo ACHANA NA MIL 5 ZA RAIS SAMIA…KUMBE MASTAA SIMBA WAMEPOTEZA ZAIDI YA...

ACHANA NA MIL 5 ZA RAIS SAMIA…KUMBE MASTAA SIMBA WAMEPOTEZA ZAIDI YA MIL 300…

Habari za Simba

Achana na ahadi ya Sh 5 Milioni kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Saluhu Hassani kama wangefunga bao mbele ya Raja Casablanca, mastaa wa Simba wakiongozwa na Clatous Chama, Moses Phiri na John Bocco wamepishana na fuko la fedha.

Rais Samia aliahidi kununua kila bao kwa Sh5 Milioni, lakini Simba ilijikuta ikipoteza kwa mabao 3-0 kwa Wamorocco na kuzikosa fedha hizo, lakini walikuwa na ofa nyingine ya mamilioni ya fedha kutoka kwa Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed ‘MO’ Dewji.

Mo Dewji aliwawekea mezani kina Chama Sh 300 Milioni kama timu hiyo ingeibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, baada ya kuwatembelea kambini na kuzungumza nao ili kuwahamasisha kuizima Raja Casablanca.

Siku moja kabla ya mchezo huo Mo Dewji aliwatembelea wachezaji na benchi la ufundi na kuzungumza nao kabla ya kuweka ahadi ya bonasi hiyo akitaka washinde ili kutengeneza nafasi nzuri kutoka Kundi C kwenda robo fainali ya michuano hiyo ya CAF.

Utaratibu wa Simba wachezaji wakiwekea bonasi ya ushindi wangezikomba zote kama wangepata sare basi wangetoka na nusu ya mkwanja huo, lakini kwa kupoteza wamezikosa.

Kazi kwa kina Chama sasa imebaki kwenye mechi nne zilizosalia kuhakikisha wanapambana ili washinde na kuivusha timu robo fainali kama walivyoelezwa na Mo Dewji aliyewasisitiza kwenye kikao hicho kwamba ni lazima wapambane wapite hapo msimu huu.

Simba inaifuata Vipers ya Uganda kwenye mechi ya tatu ya kundi hilo wikiendi hii kabla ya kurudiana nao mapema mwezi ujao na siku 10 baadae kuikaribisha Horoya ya Guinea iliyowatoa nishai ugenini kwa kuwafunga bao 1-0 na kumalizia ratiba yake kwa kwenda kurudiana na Raja.

SOMA NA HII  KUMBE SIMBA WALITAKA WENYEWE KUTOLEWA NA AL AHLY