Home Uncategorized KIUNGO WA RWANDA AIPA USHINDI SIMBA YA MBELGIJ MBELE YA UD SONGO,...

KIUNGO WA RWANDA AIPA USHINDI SIMBA YA MBELGIJ MBELE YA UD SONGO, ATAJA SABABU


KIUNGO wa zamani wa timu ya Simba Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa anakipiga timu ya AS Kigali ya Rwanda amesema kuwa nafasi ya Simba kushinda kwenye mchezo wa marudio dhidi ya UD Songo ni kubwa.

Niyonzima amesema anatambua namna Kocha Mkuu, Patrick Aussems alivyo na mbinu nyingi na kali katika kutafuta matokeo.

“Namtambua Kocha, Aussems yupo vizuri kwenye mbinu za kutafuta matokeo, pia mbali naye mashabiki wa Simba wanaipenda timu yao na wemgi hujitokeza kuipa sapoti.

“Kama ambavyo ilikuwa kwetu msimu uliopita naamini msimu huu itakuwa kazi kubwa kwa Simba kupenya na kuweka rekodi inawezekana,” amesema.

Simba itamenyana na UD Songo Jumapili uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa marudio wa kimataifa baada ya ule wa awali kulazimisha sare ya bila kufungana.

SOMA NA HII  VIDEO:HIKI HAPA ALICHOKIFANYA MLINDA MLANGO WA YANGA KWENYE MECHI DHIDI YA SIMBA