Home Habari za michezo MBRAZILI SIMBA MAMBO YAWA ‘JIWE’…APEWA DAKIKA 270 ZA KUJITETEA….LA SIVYO KUMKUTA YA...

MBRAZILI SIMBA MAMBO YAWA ‘JIWE’…APEWA DAKIKA 270 ZA KUJITETEA….LA SIVYO KUMKUTA YA ‘KANGA’…

Habari za Simba SC

Imeelezwa kuwa hatma ya Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ipo katika michezo miwili ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mmoja wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba ina malengo mawili katika msimu huu ambayo ni kubeba kombe la ligi na FA sambamba na kufuzu hatua ya robo fainali kimataifa.

Timu hiyo, katika Kundi lao, C ipo mkiani wakiwa hawana pointi ambapo wamepoteza mechi mbili za kwanza walizocheza, walianza kwa kufunga bao 1-0 na Horoya kabla ya kuchapwa 3-0 na Raja Casablanca.

Taarifa inasema  kwamba, kocha huyo amepewa michezo hiyo mitatu watakayoicheza Simba wa kwanza ni wa ligi dhidi ya Azam FC ambapo walitoka sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa mingine miwili ya kimataifa dhidi ya Vipers SC ya Uganda ambao Simba watakuwa wageni utakaochezwa nchini Uganda kabla ya kurudiana na timu hiyo, nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa.

“Simba wanataka heshima katika msimu huu, hivyo Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, walimuwekea malengo katika mkataba wake kabla ya kuusaini.

“Mingine hii miwili inayofutia ya mfululizo dhidi ya Vipers tutakaoanzia ugenini na nyumbani ambayo lazima yote tushinde ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu ribo fainali kimataifa, hivyo kocha ni lazima apambane na benchi la ufundi kuhakikisha tunashinda michezo yote hiyo ili ajiweke salama,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kocha huyo juzi alizungumzia matokeo mabaya waliyoyapata dhidi ya Horoya AC na Raja Casablanca na kusema kuwa “Nimejipanga kupata matokeo mazuri ya ushindi dhidi ya Vipers tutakapocheza ugenini kabla ya kurudiana nyumbani.

“Lakini ninahitaji muda zaidi wa kuijenga timu imara na kutumia, kwani tangu nimejiunga na Simba kupata muda mwingi wa kuandaa timu na badala yake kucheza michezo ya mfululizo bila kupumzika,” alisema Robertinho.

SOMA NA HII  ZAWADI ZATOLEWA KWA MASHABIKI NA SPOTI XTRA