Home Habari za michezo UTAFURUKUTA WEEE…LAKINI ZIKIFIKA DK HIZI…SAKHO LAZIMA AKUTUNGUE AISEE…

UTAFURUKUTA WEEE…LAKINI ZIKIFIKA DK HIZI…SAKHO LAZIMA AKUTUNGUE AISEE…

Habari za Simba

Winga wa Simba, Pape Sakho ametupia mabao saba kwenye Ligi Kuu Bara akiwa mchezaji wa nne mwenye mabao mengi ndani ya kikosi hicho akiongozwa na Mosses Phiri na Said Ntibazonkiza ‘Saido’ wote mabao 10 huku John Bocco akiwa na mabao tisa.

Sakho huu ni msimu wake wa pili ndani ya wanamsimbazi hao ambao msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na mabao sita huku, George Mpole wa Geita akiibuka mfungaji bora kwa mabao 17.

Katika mabao sita ya msimu uliopita, matatu alifunga kipindi cha kwanza na matatu akifunga kipindi cha pili tofauti na msimu huu mabao yote saba amefunga kipindi cha pili na matano akifunga akiwa nyumbani Uwanja wa Mkapa.

Bao lake la kwanza alifunga kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar siku ambayo alitupia kambani mabao mawili, bao la tatu akifunga dhidi ya Ihefu kwenye uwanja huo.

Sakho mabao ambayo amefunga ugenini ilikuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Simba ikiichapa 5-0 Geita Gold siku ambayo alifunga mabao mawili na mabao mengine yakifunga na Bocco, Clatous Chama pamoja na Kibu Denis.

Mabao mengine alifunga mchezo dhidi ya Mbeya City kisha akitupia bao la kideoni mechi iliopita dhidi ya Singida Big Stars na kuifanya Simba kushinda mabao 3-1.

Msenegali huyo msimu uliopita bao lake dhidi ya ASEC Mimosas liliibuka bao bora la CAF na kumshinda, Gabadinho Mhango wa Orlando Pirates na Zouhair El Moutaraji wa Wydad Athletic.

Wikiendi hii Sakho atakuwa na jukumu zito Simba itakapokuwa ugenini dhidi ya Horoya ya Guinea kwenye mchezo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Msimu uliopita akiwa Caf alifunga mabao mawili pekee yote Uwanja wa Mkapa kwani bao lingine alifunga mchezo dhidi ya RS Berkane Marchi 13 mwaka jana Simba ikishinda bao 1-0.

Kabla ya kusajiliwa Simba, Sakho ameichezea Teungueth FC, Mbour P.C na Diambars FC zote za Senegal pia ameichezea Noisy-le-Grand ya Ufaransa.

SOMA NA HII  JEMBE LA BENCHIKHA NDANI YA SIMBA LATAJA SIKU YA KURUDI RASMI KUKIWASHA.....