Home Habari za michezo YANGA WAMSHUTUKIA METACHA….WAMPIGA MARUFUKU KUNYWA POMBE…KUKATWA MIL 1….

YANGA WAMSHUTUKIA METACHA….WAMPIGA MARUFUKU KUNYWA POMBE…KUKATWA MIL 1….

Habari za Yanga

Wakati kipa wa Yanga, Metacha Mnata akiendelea na majukumu yake kikosini humo, uongozi na benchi la ufundi la timu hiyo limemtaka kuachana kabisa na matumizi ya kinywaji cha aina yoyote ambacho kitaweza kumchanganya kichwa na kusababisha afanye makosa mapya kwa wenzake.

Metacha alitua Yanga kwa mkopo katika usajili wa dirisha dogo la usajili akitokea Singida Big Stars kwenda kuziba nafasi ya kipa namba mbili Aboutwalib Mshery ambaye aliumia mazoezini na kutakiwa kuwa nje kwa miezi miwili hadi sita muda mchache kabla ya dirisha kufungwa.

Chanzo chetu kutoka kambi ya Yanga kimesema kuwa, mabosi wa Yanga na benchi la ufundi kwa ujumla wake, umemtaka Metacha kutosababisha kosa lolote la utovu wa nidhamu wala kusikika akiwa amekunywa kinywaji chochote cha kumvuruga akili, akiwa kikosini au wakati wa mapumziko.

“Kwenye mkataba wa miezi sita alioingia na sisi Metacha hatakiwi kuonekana amefanya jambo lolote la kiutovu wa nidhamu na endapo akifanya anaweza kukatwa hadi nusu ya mshahara wake au zaidi ya nusu, ila pia amepangiwa idadi ya pesa pale akisababisha kosa la kuigharimu timu akiwa mchezoni.

“Kosa la kuchelewa mazoezini anaweza kukatwa zaidi ya milioni moja lakini akichelewa kambini pia anaweza kukatwa zaidi ya hiyo na akionekana kalewa kambini anaweza kufukuzwa kabisa au kusimamishwa, ila pia amepewa kipengele cha kuwa mfano bora ili kama atatimiza hilo uongozi unaweza kumuongezea mkataba na kipa mmoja akaachwa kwneye dirisha kubwa,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- ILI KESHO TUSHINDE....WACHEZAJI WAPEWE iPhone 15 na MIL 100 KILA MMOJA...