Home Habari za michezo GAMONDI:- HATA TUKIKUFANGA GOLI 5…TUTAENDELEA KUKUSHAMBULIA TU….

GAMONDI:- HATA TUKIKUFANGA GOLI 5…TUTAENDELEA KUKUSHAMBULIA TU….

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema kuwa falsafa ya soka lake ni la kuburudisha hata kama itatokea anapoteza mchezo.

Gamondi ameingia kwenye vitabu vya Historia mpya ya Klabu ya Wananchi Yanga SC kwa kushinda bao 5 katika mechi nane ndani ya msimu wake wa kwanza tu kwenye timu hiyo.

“Ni bora unifunge kuliko nikuonyeshe udhaifu tena nyumbani kwangu, mimi mpira ni burudani nataka niburudishe halafu nishinde, ikitokea nimeshindwa basi nitakuwa nimeburudisha na ikitokea nimeshinda na kuburudisha pia.

“Siwezi kucheza na mabeki 9 halafu mshambuliaji mmoja hata kama naongoza kwa mabao matano nitaendelea kukushambulia tu,” amesema Kocha Miguel Gamondi.

◉ Yanga 5 – 0 KMC
◉ Yanga 5 – 0 JKT Tanzania
◉ Yanga 5 – 1 ASAS
◉ Yanga 5 – 1 Simba SC
◉ Yanga 5 – 0 Jamhuri
◉ Yanga 5 – 1 Hausing FC
◉ Yanga 5 – 0 Polisi Tanzania
◉ Yanga 5 – 0 Ihefu FC.

Mechi inayofuata ni Yanga dhidi ya Geita Gold FC.

Pengine Miguel Gamondi ndiye kocha katili zaidi kwenye historia ya Yanga SC?

SOMA NA HII  KAZI ZA 'KIKATILI' ZA MCHEZAJI WA YANGA ZAMFANYA KIGOGO WA TFF KUIBUKA NA HILI..ATOA ONYO...